Kamwe sitounyamazia huu Upuuzi wa baadhi ya Mashabiki Wenzangu wa Simba SC kuwa GSM imedhamini Vilabu Saba NBC hivyo itapanga Matokeo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sasa kama mnajua kuwa GSM ambao ndiyo Wadhamini Wakuu wa Yanga SC na kwamba itasababisha Fikra zenu za Kipumbavu kuwa kutakuwa na Upangaji wa Matokeo (Match Fixing) pale Yanga SC ikicheza na hivyo Vilabu Saba ( 7 ) sasa kwanini nanyi / nasi pia tusimwambie Tajiri yetu Tapeli na Muongo nae amalizie kwa Kuvidhamini hivyo Vilabu vingine Saba au Nane vilvyobaki ili nasi tupange Matokeo tuwe Mabingwa?

Hamna Akili kabisa nyie yaani mnaacha / tunaacha Kulia na Uozo mkubwa unaoanzia katika Uongozi, Benchi la Ufundi, Wachezaji na hata Sisi Mashabiki / Wanachama tunaanza Kukimbilia kusema kuwa GSM na Yanga SC wanapanga Matokeo kwa Kuvinunua Vilabu na mpaka Waamuzi wa Ligi Kuu.

Hebu Mashabiki Wenzangu wa Simba SC nawaombeni Leo tuweke Unafiki na Upumbavu wetu pembeni na tuulizane haya Maswali. Hivi kweli tukitulia kabisa tukiwaangalia Wachezaji wa Yanga SC, Makocha wao, Utawala / Uongozi Wao, Mfumo wao mzima wa Kiutendaji, Idara zao zilivyo,Ufanisi na Morali yao kuanzia kwa Mashabiki hadi Mashabiki walionao unafanana na Sisi Simba SC yetu?

Soma Pia: Mdhamini mkuu wa Yanga GSM kudhamini timu nyingine saba za ligi kuu siyo fair

Kiutani wetu wa Simba na Yanga Mimi GENTAMYCINE huwa napenda sana Kuwatania wana Yanga SC wote hapa JamiiForums ili tu Kuchangamshana na Kudumisha ule Utamaduni wetu wa Utani wa Jadi ila kiukweli na nikivaa sasa Viatu vya Mwanamichezo na Mchambuzi na ambaye pia naijua Sayansi ya Mpira ilivyo siogopi na wala sioni Aibu kusema kuwa Yanga SC wameshatuacha mbali, wapo vyema, wanajua wanachokifanya, wala hawahongi Waamuzi au TFF bali Continuity Performance yao ndiyo inawabeba.

Mwisho nashauri huu muda ambao Sisi Wapuuzi ( wana Simba SC nami GENTAMYCINE nikiwemo ) ambao Kutwa tunautumia Kuwalaumu GSM na Klabu ya Yanga kuwa Wanahonga tuutumie Kuuhoji Uongozi wetu kuwa ni kwanini kila mwaka wanafanya betting katika Usajili wa Wachezaji wetu na pia kwanini Klabu ya Simba inaendeshwa Kienyeji Kienyeji, Kishikaji, Kiunafiki na kuna Wapigaji ( Wazee wa 10% wengi sana ) na hakuna Umoja baina ya Uongozi na Sisi Mashabiki?

GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE Mzee wa DOZI TUKUKA nimemaliza na kwa wale ambao MTANICHUKIA kwa huu Ukweli wangu wala sijali, ila Siku zote nitabakia kuwa Mkweli, Muwazi na kamwe sitokubali kuwa Mnafiki au Muongo ili tu niitetee Klabu yangu ambayo kila Siku naiona inadidimia tu huku Wapuuzi wengi wakiwa wala hawalioni hilo na badala yake Wanadanganywa tu na Comedy za Msemaji wetu wa hovyo.

Tujitafakari na Tujitathmini sana kwani bado hatujachelewa japo kwa kuwa Mabingwa Msimu huu tumeshachelewa.
 
popoma linalojielewa hilo..😁

karibuni young African,tuwafundishe namna yakuendesha timu wapi mkazie idara zipi ni muhimu na namna yakubehave na wachezaji,na ni kivipi utapata wachezaji bora.
kama hamtaki tutaendelea kuwawekea misumari,chakaza sana mpoteane!.
 
Genta! Chukua soda kwa Mangi nakuja kulipa☺️
 
Afadhari wewe umeongea labda watasikia maana chawa ni wagumu kuelewa jana nmeuliza humu hii timu inaendeshwaje mwaka wa pili bila mkutano mkuu wala kusomewa budget mazuzu yakanishambulia
 
Kama unaelewa mambo utaona kuna tatizo kama huelewi huwezi ona tatizo
 
Kama unaelewa mambo utaona kuna tatizo kama huelewi huwezi ona tatizo
Kabisa umechunguza mwenendo wa Yanga akicheza mechi za ligi, akicheza na Simba isiyodhaminiwa na Gsm, akichekeza na Mamelodi isiyodhaminiwa na Gsm, akicheza na Al Ahly isiyodhaminiwa na GSM, Belouzdad, Tp Mazembe nk na bado ukaelewa kuna TATIZO.

Samahani kama nakukosea ila ushabiki wa bila kureason ni ushabiki wa kipumbavu.
 
Siwawahi kuona moja ya mashariti ya udhamini ni kuachia timu flani ikufunge hii kitu inasukumwa na mashabiki machawa kufunika uozo uliopo kwenye club
 
Hili sikuwa nalijua kwakweli.
 
Hatuachi kusema na tutasema tuu labda mtupake super glue mdomoni....
leo nikakutana na mdada wa simba kumtania kidogo tu akashika mawe! na nilikuwa mbali kidogo nae nilimsogelea ghafla!,akanikosakosa jiwe la kwenye kizazi sasahivi mnamakasiriko ndo mmefikia level hii duh!..😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…