Kamwe usijaribu kumng’ang’ania mwanamke anayeonekana hakuhitaji tena, utaumia

Bata batani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
3,217
Reaction score
3,694
Naandika wosia huu kwa vijana wenzangu baada ya kupona maumivu ya kuachana na mwanamke niliempenda sana miezi kadhaa iliyopitaa ila kitu nilichojifunza mwanamke akionekana ameonesha dalili hakuhitaji tena.

Mwanamke akifikia hatua amekubadilikia na akaonesha dalili za kutaka kuachana na wewe ni bora ukubali matokeo mapema kabla haujafikia hatua ya suffering na stress kwani maumivu yake ni makali zaidi ukiwa ndani ya uhusiano kuliko njee ya uhusiano

Mwanamke akiwa hakuhitaji tena penzi utaliona chungu, dharau kibao, utaishi kwa stress huku ukijiwazia huyu kapata mwingine nini kwani atakutesa mnoo, kitu kidogo ugomvi, maneno.

Ushauri wangu kwa vijana chonde chonde ukiona mabadiliko ya kitabia kwa mwanamke wako ambayo huyaelewi elewi zungumza nae ukiona haelekei kaa nae mbali, ikiwezekana mapema mnoo funga ukurasa kila mtu Asepe na maisha yake, nina mengi ya kusema.
 
Ulichokiongea ni sahihi shida huwa inakuja huwa ni moyo..... Usipoweza kuzisimamia hisia zako lazima uwe zoba,

Kama mwanaume unapaswa kujipiga kifua na maisha kuendelea, usiruhusu kusikiliza ya upande wa pili.. wala kuletswa story zake

Unapoamua kumuacha hakikisha kuwa umejiridhisha kuwa unasababu ya kumuacha
 
Hivi mbona tunaolalamika sana kuachwa ni sisi me..?
Wanawake tumewakosea nini..?
Na hii hali itaisha lini..?

Mtafanya nimuamini moja ya mwanasaikolojia alienena kuwa wanaume tupo sensitive sana na mapenzi japo tunajifanyaga makauzu ila hapo tumeshikika!
 

Mimi kwa kwelii kipindi mwanamke wangu kuna mambo matatu nilikuwa najitahidi kuyafanya ili nisimpoteze mpenzi wangu

1. Nilijitahidi sana kufanya mambo yote anayoyataka yeye ili moyo wake uridhike

2. Nilijitahidi kuonyesha moyo wangu unampenda, nilijitoa kwake ili nisimpoteze

3. Nikimkosea kidogo najitahidi kuomba msamaha

Ila mwisho wa game nilianza kujiona mjinga kwani dharau zilizidi hatari ilifikia hatua hata mimi na yeye kuongozana barabarani njia moja hataki kila mtu atembee kivyake kama hatujuani.

Siku ambayo nakuja kufanya maamuzi magumu ya kuanza kujitoa kwenye penzi lake ni baada ya kupewa story chini ya kapeti mwanamke wangu anatafuta Chumba ajee kuhama kimya kimya hapo ndo nilipogundua sipedwiiiii
 
Mapenzi bwana acha hawa viumbe, bwana akionyesha dalili hata usitake suluhu huko ni kujichosha sana,

Unapaswa tu utafute mlango wa kutokea maisha ya endeleee huwa inaumiza unakuta umeshamtolea na mahari
 
Achaaa kabisa Hebu fikiria mwanamke wako hata kuongozana na wewe njia moja hatakiii .
Mimi alinifokea kwasababu nilimtumia hela baada ya yeye kusema anahitaji pesa then nikamkumbusha namhitaji nna miezi miwili sijala mzigo.

Aliponikasirikia (eti tatizo namkumbusha wakati gani, inakuwa kama tunauziana kitu) ndio nikashtuka kumbe hapa sina mwanamke anymore.
 

Nilichogundua sisi wanaume tunaolalamika kuumizwa ni kwamba tunakosea sehemu moja

Tukipedwa na wanawake huwa tunajisahau sana tuwaamini sana watoto wa kike lakini siku wakitubalikia tunajifanya tunambeleza tunaomba msamaha mwisho wa siku nothing changes

Ni maumivu tuu
 
Hayo matatu yote yalikuwa makosa! Hata kama unampenda vipi unatakiwa kuuchuna kiaina asijue kuwa umeoza!!.. hawa viumbe haitakiwi kuwaonyesha unawapenda sanaaaa!
 
Mapemzi bwana acha hawa viumbe , bwana akionyesha dalili hata usitake suruhu huko ni kujichosha sana ,

Unapaswa tu utafute mlango wa kutokea maisha ya endeleee huwa inaumiza unakuta umeshamtolea na mahari

Kabisaa ukijifanya mbishi utazidi kuumia

Mimi kipindi natafuta mlango wa kutokea niliangaika sana nifanyeje ila nashukuru kuna mtu alinisaidia sana nilianza taratibu sana

Kabla ya yote nilimwita nizungumze nae nilijifanya Lofa ili nijue msimamo wake

Nilivyogundua hapa napoteza muda nilianza taratibu mnoo huku nikimwomba Mungu anivushe hatua hiii
 


Jibu rahisi ni kwamba,
Mademu wana options nyingi ambapo mwanaume wa kawaida hana, mwanamke kupata mwanaume ni rahisi lakini kwa mwanaume kupata demu hasa demu anayemtaka ni ishu, kwa maana ni lazima huyo demu akubali kwanza, ...
 
Hayo matatu yote yalikuwa makosa! Hata kama unampenda vipi unatakiwa kuuchuna kiaina asijue kuwa umeoza!!.. hawa viumbe haitakiwi kuwaonyesha unawapenda sanaaaa!

Yes brother na hapo ndipo nilipokosea

Yaani nilivyojifanya mzee wa kuomba msamaha

Mzeee wa upendo kumbe ndo nazidi kumpa moto wa kuniona mimi boya
 
Hata Mimi ningefoka ungesubiri hata baadae kidogo sasa wewe hapohapo[emoji23]
 
Kweli kabisa inaumiza sana, unakuta umempenda mtoto wa mtu kumbe yeye anakuchukulia powah.

Wanaume tunakazi sana ndio maana tunakufa haraka
Alafu unakuta umetumia nguvu ya pesa nyingi kuwa nae lakini mwenyewe hata habari na wewe hana! Hapo ndiyo naaminigi kuwa Mapenzi siyo pesa, maana hao wenye pesa ndiyo wanateswa sana na mapenzi ukilinganisha na watu wa vipato vya chini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…