kitoto wa vitoto
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 375
- 410
Naomba usome kidogo!!!
Hii ni real siyo utani!
Mimi ni kijana wa miaka 32
Mnamo mwaka 2014 nilitoka nyumbani rasmi kuja mjini kutafuta maisha, Niliaga vizuri wazazi wangu nikawaahidi kuwa naenda mjini na nitapokelewa na rafiki yangu na ndie nitakayeishi nae.
Nilifika mjini na begi yangu ndogo iliyoandikwa "unibest". Baada ya kufika mjini mwenyeji wangu alinitelekeza stand bila kosa Wala huruma.
Nilimpigia mara kadhaa Ila hakupokea simu mwishowe ikazimwa, Nilikaa stand Hadi saa sita usiku nikiwa na matumaini labda atanipigia au kunifuata.
Muda ulienda hakutokea nikapata wazo la kutafuta rafiki yangu mwingine ambae nilisoma naye shule ya msingi akinitangulia madarasa 2 mbele. Nilimueleza kisa chote, akanipa pole na akaahidi atakuja kunichukua stend alikuwa anafanya kazi ya kuchoma nyama hivyo alikuja kunichukua saa nane usiku.
Nilifurahi na nilishukuru sana nilikaa nae kwa muda nikawa natafuta kazi kwa bidii, nilipata kazi ya mshahara mdogo sana ya 100,000 kwa mwezi sikujali, sikuangalia nimesoma au sikusoma nilipambana nayo. Nilifanya kazi mithili ya mchwa, nilitaka chochunga nisimuaribie mtu kazi kutokana na bidii yangu, "nisiwe chawa wa boss" Nilibahatika kuongezewa mshahara kidogo.
Nikafanya miezi 8 nikafungua biashara yangu ndogo nilikuwa nasave 5000 kila siku Bora nisile, baada ya muda huku nikiendelea na kazi yangu ile ile ya mwanzo biashara yangu ilizidi kupata kibali ikakua kadri siku zinavyozidi kwenda, nilifanikiwa kusave 12,000 kwa siku nikichangaya na mshahara nikawa kwa mwezi Nina kitu kama laki 5. Sikukata tamaa Wala kubweteka, niliendelea na kazi kwa bidii ile ile tena kwa nidhamu ya juu.
Nilipata dada mmoja aliyekuwa akifanya kazi za ndani Ila alikuwa akipitia manyanyaso sana alikuwa akilala usiku wa saa nane boss wake alikuwa mnywaji hivyo alikuwa halali mpaka amfungulie geti na kuamka saa kumi na nusu kila siku.
Sikupenda Yale maisha kwa ujumla muda mwingi watoto wa boss Wanamdharau dah nilitokea kumuelewa nilimchunguza nikagundua hakuwa na ujuzi wowote japo alifaulu kwa alama nzuri kidato Cha nne. Akiwa Hana hata ujuzi wowote nilimpenda nikampeleka shule akaenda somea ujuzi.
Baada ya hapo nilimuoa na Sasa ni mke wangu.
Baada ya kuhitimu nilimfungulia biashara.
Hadi Sasa anafanya vizuri tu.
Mungu ni mkubwa
Mimi ninaendelea na kazi ile ile ya mwanzo Hadi leo hii. Ila kwenye biashara mungu ameniinua kwa kiasi nimefungua na branch hivyo mimi kwa sasa nasave 50k kwa siku na mke wangu anasave 35k kwa siku,
Kazini pia napokea mshahara kila mwezi.
Nina bustani ya mboga mboga, hoho za aina zote nauza kwenye hotel za kitalii mwenyewe,
LENGO LA KUANDIKA HUU UJUMBE
Sijaandika huu ujumbe kwa ajili ya kuwafafanulia au kuwatambia Kwa namna yoyote ile Bali kukutia moyo ewe rafiki yangu ambaye umekata tamaa kabisa pengine mshahara ni mdogo na unataka kuacha kazi kamwe jiongeze huko huko
Muombe mungu akupe mambo makuu matatu
1: Mtu sahihi wa kukushauri /mke/mume
2: Moyo usiobweteka Wala kukata tamaa
3: Sehemu sahihi ya kukuongezea kipato/biashara
Hayo yote yatafanikiwa endapo tu utakuwa ni mtu wa kushukuru japo kwa kidogo, fungu la kumi na sadaka ni jambo muhimu sana, Pia kuwa mtu wa haki kuanzia kazini unakofanya hadi nyumbani unakoishi
Ukiita Mungu Mungu ataitika muda huo huo na utaongea naye naye Mungu atakuitikia
Mungu awabariki