Kanali masawe,bwana afya na afisa bishara manispaa bukoba pamoja na tra kagera mko wapi?

Kanali masawe,bwana afya na afisa bishara manispaa bukoba pamoja na tra kagera mko wapi?

mukama talemwa

Senior Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
160
Reaction score
29
Baada ya Kanali Masawe kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera alikuja na mikakati mingi hasa ya kuhakikisha mji unakuwa msafi, na kwa hilo alifanikiwa sana na akapanga siku ya alhamisi kuwa siku rasimi ya usafi,Mji ulipendeza ukawa safi sana,kiasi cha kuwa mfano kwa miji mingine.
Ila kitu cha kusikitisha kwasasa mji umekuwa mchafu, nenda kwenye vyoo vya stand utakuta hali mbaya hata zile tiles zilizowekwa zimeanza kubadirika rangi.Standi yenyewe ni matope matupu ingawaje kila gari linalopakia na kutelemsha abiria lazima alipe, sasa hizo pesa za kazi gani?
Uchafu ninavyojua mimi nikitu chochote ambacho hakiko katika nafasi yake yaani kimewekwa hovyohovyo.Sasa hapa Bukoba mjini watu wamegeuza sehemu za watembea kwa miguu kuwa maduka kitu ambacho kwa uelewa wangu nayenyewe ni uchafu.Nimetaja TRA pamoja na aofisi ya biashara ya manispaa kwa kuwa hayo maduka yaliyojaa barabarani haya leseni wa hayalipi mapato sasa tunajiuliza kwanini? au niyahao maofisa?Haya maduka ni ya mitaji mikubwa wanauza viatu kwa wingi vyombo vya ndani,masanduku kwahiyo mitaji yao ni mikubwa,lakini chakusikitisha ukiwa na kakibanda (kiosk) tu cha mtaji wa laki 2 hadi 3 TRA pamoja na watu leseni lazima wakutake ukate leseni pamoja kulipia mapato,sasa wanataka watu wote wapange bidhaa zao barabarani? watoeni hao ili tushinde kwa usawa.Tatizo jingine kitendo cha kuwaacha wakafanyabishara zao pale kwa muda mrefu wanajiararishia kukaa maeneo yale siku serikali ikitaka kuwatoa ni vita,tumeyashuhudia haya sehemu nyingine za miji,kwahiyo kwanini wasitolewe mapema ili kuepusha hayo?
Pili kwakuwa wao hawalipi chochote kiushindani wa kibiashara kuna watu wanaumizwa wale wanaolipia chumba,leseni, mapato,tozo ya kuzoa taka ada ya matangazo kwa kuandika jina kiosk chake.
Manispaa wako bussy kukusanya mapato lakini wameshindwa hata kurudishia zile alama za watembea kwa miguu.
Niombi langu kwa maofisa hawa kila mtu kuwajibika kwa sehemu yake ili Serikali ipate mapato na mji wetu uendelee kuwa msafi.
 
Back
Top Bottom