Kanda ya ziwa badilikeni

Kanda ya ziwa badilikeni

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Wakati mwingine watu wanasema kiutani lakini tunaomba kanda ya ziwa wabadilishe tabia zao ambazo si za maendeleo. Utamaduni wa uchawi na ndoa za utototoni zinarudisha sana maendeleo ya sehemu ambayo ina watu wengi, madini, ziwa na nafasi za kulima mazao mengi. Mkienda vijijini waelezeni wazee waache hizi tabia tunataka watoto wa kike wasome na albino wasiogope kuuliwa kwasababu tu wamezaliwa na kilema. Wakati mwingine kusemana si kubaya.

Tanzania. In Tanzania, albinos represent one in every 1429 births, a much higher rate than in any other nation. ... Albinos are especially persecuted in Shinyanga and Mwanza, where witch doctors have promoted a belief in the potential magical and superstitious properties of albinos' body parts

Ndoa utotoni
Shinyanga ukiongoza kwa 59%, ukifuatiwa na Tabora 58%, Mara 55%, Dodoma 51%, Lindi 48%. Mwanza 37%
 
Ni kwasababu ya mazingira mabovu wa shule zetu.

Shule zetu zingekuwa zina mazingira mazuri na wanafunzi wanafaulu, tatizo la watoto wa shule kupata mimba au kuolewa wakiwa na umri mdogo lisingekuwa kubwa.

Maeneo mengine huko vijijini, na haswa yale ambayo ni notorious kwa kupachika wanafunzi mimba, kwenda shule ni sawa na kwenda kuzurura.
 
Mkuu mbona hizo takwimu zako hazionyeshi kitu kinacholinganishwa, mfano tukijumlisha shinyanga na tabora tayari zinavuka 100%. Tunaomba kujua ni data zipi zimewekwa kwenye numerator na denominator hadi kuweza ku calculate hizo percentages na ungetuwekea takwimu za mikoa yote ili tuweze kufanya ulinganifu ambao ni objective zaidi.

Unaposema utamaduni wa uchawi unakuwa reflected na mauaji ya albino, unataka tuamini kuwa mikoa ambayo haina matukio ya mauaji ya albino hakuna uchawi?

Mbona maeneo mengine kibao ambayo hayapo kanda ya ziwa tumesikia matukio ya ushirikina, mfano kuchuna ngozi kule mbeya, ishu za sumbawanga na maeneo ya kusini mfano, ruangwa na yale matukio ya kwenda kutambika kila mwaka kule kaskazini, au kinachofanyika huko kwengine hakiitwi uchawi, labda tuseme ni ushirikina...
 
Mkuu mbona hizo takwimu zako hazionyeshi kitu kinacholinganishwa, mfano tukijumlisha shinyanga na tabora tayari zinavuka 100%. Tunaomba kujua ni data zipi zimewekwa kwenye numerator na denominator hadi kuweza ku calculate hizo percentages na ungetuwekea takwimu za mikoa yote ili tuweze kufanya ulinganifu ambao ni objective zaidi. Unaposema utamaduni wa uchawi unakuwa reflected na mauaji ya albino, unataka tuamini kuwa mikoa ambayo haina matukio ya mauaji ya albino hakuna uchawi? mbona maeneo mengine kibao ambayo hayapo kanda ya ziwa tumesikia matukio ya ushirikina, mfano kuchuna ngozi kule mbeya, ishu za sumbawanga na maeneo ya kusini mfano, ruangwa na yale matukio ya kwenda kutambika kila mwaka kule kaskazini, au kinachofanyika huko kwengine hakiitwi uchawi, labda tuseme ni ushirikina...

..kama unataka kujadili wachuna ngozi, wakeketaji, etc etc wafungulie thread muhususi kwa ajili yao.

..hapa unatakiwa ujadili mada na hoja zilizoko mezani.

NB.

..watawala badala ya kujenga MABWENI ili watoto wa kike wasome kwa usalama wananunua NDEGE kwa kutumia KODI za wananchi MASIKINI.
 
Mti wenye matunda ndio unaopigwa na mawe
Kanda ya ziwa inawaumiza vichwa sana Mpaka mnaweweseka , Kila kukicha mnawashambulia wakati wao wako kimya busy na kazi, Mmetawaliwa na ukabila na ukanda mpaka mmekuwa kero
Hakuna ukanda sifa ya umoja wa kijamaa kama kanda ya ziwa makabila yote ya watafutaji yanapatikana huko
 
Tanzania. In Tanzania, albinos represent one in every 1429 births, a much higher rate than in any other nation. ... Albinos are especially persecuted in Shinyanga and Mwanza, where witch doctors have promoted a belief in the potential magical and superstitious properties of albinos' body parts
Hili mbona rahisi kulidhibiti; kwa nini liwe tatizo.

Tuwalete 'mabeberu' wawe mbadala, kwani hawawezi kuwa 'substitution' nzuri kwa albino, ambao kiukweli ni ndugu zetu?

Tutakuwa tumemaliza matatizo mawili kwa mpigo, kama vile "kuua ndege wawili kwa jiwe moja."

Tatizo la kwanza ni - ubeberu wao
Tatizo la pili ni - kuwasitiri ndugu zetu albino.

Au unasemaje mkuu 'Kamundu'

Mada hizi za kulenga sehemu fulani palipo na tatizo inaonekana ziko ndani ya damu na mioyo yenu. Ni tatizo ambalo hamuwezi kuachana nalo, ni sehemu ya maisha yenu kama ilivyo kule nyumbani mlipoanzia maisha yenu hapa duniani.
 
Huu ni ukabila!.
P
Kama unashaka, iondoe.
Na matatizo sasa yanakuwa kwamba watu waliohamia, pakiwemo wakimbizi na wengine ambao tumewapa uraia wa nchi yetu ndio watakuwa mbele kutafuta mifarakano kati yetu.

Baadhi ya watu hawa inabidi wanyang'anywe walichopewa kama hawawezi kuishi nasi na kuachana na mifarakanyo ya huko walikotoka.

Hili nalisema kwa moyo mzito, kwa sababu halistahili kamwe kuwa tatizo. Lakini tukilifumbia macho litatumaliza sote.
 
Kwenye asilimia ni asilimia ya idadi ya watoto wa pale sio asilimia ya Tanzania nzima. Kuonyesha ni idadi gani ya watoto kati ya wote waliopo hizo sehemu wanaolewa utotoni
 
Hizo namba hazifanganyi niiteni chochote nitasimama kwa ukweli tu. Napinga ndoa za utotoni, kuua alibino kwa mila za kichawi na unyanyasaji mkubwa wa wanawake unaoendelea. Kama wewe hauko kwenye hilo kundi badala ya kutaa ukweli jitahidi kupigania haki za ndugu zenu. Haya yote ni kwa maendeleo ya nchi. Kuna vipaji vingi sana vya watoto wetu vinapotea kwa tamaa za wanaume na utamaduni mbaya wa ndoa za utotoni. Kanda ya ziwa kwasababu wana watu wengi ni ngumu kupunguza tatizo bila kupinguza hili tatizo kanda yetu ya ziwa. Kuweni na utamaduni wa biashara zaidi, elimu, na kujenga kwenu.
 
Mti wenye matunda ndio unaopigwa na mawe
Kanda ya ziwa inawaumiza vichwa sana Mpaka mnaweweseka , Kila kukicha mnawashambulia wakati wao wako kimya busy na kazi, Mmetawaliwa na ukabila na ukanda mpaka mmekuwa kero
Hakuna ukanda sifa ya umoja wa kijamaa kama kanda ya ziwa makabila yote ya watafutaji yanapatikana huko

Yaani kati ya watoto wote 59% shinyanga wanaolewa kabla ya miaka 18 halafu unasema ni miti! Ni matunda gani unayoongelea! Matunda ni hawa watoto ambao wanazuiwa kujiendeleza kwa mila mbovu. Kama ni matunda basi hayaja komaa bado. Hii nchi zaidi ya 50% watu hawana kazi. Mtoto akipata mimba anafukuzwa shule sasa nani kampa mimba wakati wanaolewa watoto!. Ukabila ni pale ambako hukubali ukweli kwasababu tu ni kabila lako

Niiteni beberu tena lile kubwa lakini nitakuwa upande wa watoto wa kike na kuwatetea kwasababu najua kama nchi hatuwezi kushindana kama watoto wetu hawapati elimu badala yake wanaolewa.
 
Write your reply...mnakera sana nyie wakaskazini.sie tunajiletea maendeleo wenyewe nyie mlisaidiwa na mkoloni.now tunapiga hatua mnaanza kuhamisha magoli.yaani mnataabika sana na kanda yetu afu sie wala hatusemi ya kwenu.
 
Hili mbona rahisi kulidhibiti; kwa nini liwe tatizo.

Tuwalete 'mabeberu' wawe mbadala, kwani hawawezi kuwa 'substitution' nzuri kwa albino, ambao kiukweli ni ndugu zetu?

Tutakuwa tumemaliza matatizo mawili kwa mpigo, kama vile "kuua ndege wawili kwa jiwe moja."

Tatizo la kwanza ni - ubeberu wao
Tatizo la pili ni - kuwasitiri ndugu zetu albino.

Au unasemaje mkuu 'Kamundu'

Mada hizi za kulenga sehemu fulani palipo na tatizo inaonekana ziko ndani ya damu na mioyo yenu. Ni tatizo ambalo hamuwezi kuachana nalo, ni sehemu ya maisha yenu kama ilivyo kule nyumbani mlipoanzia maisha yenu hapa duniani.

Tutoe suluhisho la matatizo badala ya madongo. Nimesema waache mila mbovu wewe unasemaje waendelee na ndoa za utotoni au ? Msimamo wako ni upi?
 
Sidhani kuwa wewe kwenye mada hii unalo suluhisho la matatizo; badala yake unachochea matatizo. Usidhani hatuelewi lengo ni nini!

Kazi ni kutambua mnachokifanya.

Usiingize watu wengine haya ni mawazo yangu binafsi ukisema “ mnachokifanya” ni kama vile kuna vikao vya siri 😂. Soluhisho langu nasema waache lakini labda watu wa huko wangeweza kusema zaidi. Huo uchawi wa kuua albino mimi nitaujuaje? Hivyo soluhisho ni watu wa kule kutoa elimu kwa ndugu zao wanaofanya hivyo asilimia 59% shinyanga kama umetoa huko utakuwa na ndugu tu ambaye ameolewa au kuoa utotoni!. Msijaribu kukwepa na kuingiza watu wengine kwenye swala hili.
 
Sidhani kuwa wewe kwenye mada hii unalo suluhisho la matatizo; badala yake unachochea matatizo. Usidhani hatuelewi lengo ni nini!

Kazi ni kutambua mnachokifanya.

..suluhisho ni kuboresha mazingira ya shule za wasichano.

..ujenzi wa mabweni ili watoto wasizurure baada ya masomo, na wapate uangalizi wa karibu utakao-improve matokeo yao, ni jambo linalotakiwa kuwa kipaumbele cha WABUNGE wa maeneo hayo.

..bila kuwaonyesha kuwa msichana anafaidika zaidi akiendelea na masomo kuliko kuolewa mapema tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.

..jambo lingine ni KUHAMASISHA / KUHABARISHA wananchi kuhusu madhara ya ndoa za utotoni na mila nyingine potofu.

..lingine ni kwamba mila potofu haziwezi kumalizwa na OUTSIDERS. kuna tatizo la kuoneana AIBU ktk kupambana na mila potofu.

..Kwa mfano, viongozi wa maeneo husika hawasikiki kukemea mila hizo, badala yake wamewaachia WANAHARAKATI ambao mara nyingi siyo wenyeji wa maeneo yaliyoathirika.

NB.

..wabunge wa kanda ya ziwa kama Joseph Msukuma, Andrew Chenge, Kishimba, Magreth Sitta, ...wanatakiwa wawe mstari wa mbele ktk suala hili. Binafsi sijawahi kuwasikia wakipaza sauti.
 
Hii topic sio dongo mfano ukiangalia vizuri kuna makabila ambayo ndugu wanagombana sana lakini vilevile ndiyo hayo yenye maendeleo. Kabla hujatoa michango ya harusi uliza jamani nani anaolewa, umri na kama ni mtoto ongea na sio tu kusema hayakuhusu mambo ya vijijini? Wachawi hawa wanajulikana lakini waelewa wanaangalia pembeni hayawahusu? Msiogope kugombana kwa maendeleo yenu. Sasa mtasema mabeberu ndiyo wanakuja kuolesha watoto au kuleta uchawi? bila aibu. Hata sisi hapa kusemana ni sawa tu ilimradi roho yako iwe na nia njema.
 
Mkuu mbona hizo takwimu zako hazionyeshi kitu kinacholinganishwa, mfano tukijumlisha shinyanga na tabora tayari zinavuka 100%. Tunaomba kujua ni data zipi zimewekwa kwenye numerator na denominator hadi kuweza ku calculate hizo percentages na ungetuwekea takwimu za mikoa yote ili tuweze kufanya ulinganifu ambao ni objective zaidi.

Unaposema utamaduni wa uchawi unakuwa reflected na mauaji ya albino, unataka tuamini kuwa mikoa ambayo haina matukio ya mauaji ya albino hakuna uchawi?

Mbona maeneo mengine kibao ambayo hayapo kanda ya ziwa tumesikia matukio ya ushirikina, mfano kuchuna ngozi kule mbeya, ishu za sumbawanga na maeneo ya kusini mfano, ruangwa na yale matukio ya kwenda kutambika kila mwaka kule kaskazini, au kinachofanyika huko kwengine hakiitwi uchawi, labda tuseme ni ushirikina...
Huko kaskazini hawaendi kutambika kila mwaka kama unavyosema. Ni kweli kuna mengi ya kubadilika kanda ya ziwa mathalani uchawi. Ni watu wachache mno kanda hii wanafanya kitu bila ndumba, hata awe professa chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom