Kanga na kelele zao

Kanga na kelele zao

spray

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
277
Reaction score
241
Habarini wana jamvi,

Kuanzia wiki iliyopita hatulali, yaani ikifika saa 10 asubuhi lazima tuamke tutake tusitake, jirani kaleta kanga wanne, yaani wanapiga kelele 24/7, kelele zilivyoanza nilijua labda ni aina flani ya bata maana kelele ni kali sana, kumbe ni kanga wale wa madoadoa, kiukweli mi napenda ufugaji lakini kwa hali hii inauzi, ukishinda nyumbani ndio utakoma, kelele mtindo mmoja kuanzia asubuhi hadi jioni.

Nimefikiria siku moja nimpe mbinu labda wasipige kelele kama nitaipata hiyo mbinu itatusaidia, maana kiukweli tunateseka mno na kelele za hawa kanga
 
Mkuu niliwahi kuwafuga zaidi ya 100. Wenye madoa madoa na weupe. Wale weupe ndio wanapiga kelele usiseme.

Nilipoamka nilitafuta mteja wa jumla waondoke siku hiyo hiyo. Hawa wanataka ufugie mbali na makazi ya watu.
 
Mpelekeni serikali ya mtaa analeta buguzi kwenye makazi ya watu.
 
Back
Top Bottom