Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,229
- 13,442
Kanga inaniuwa, kifo cha mende jamani
Kanga yanizuzuwa, hata njia siioni
Kanga iliyovaliwa, mimi huku hamkani
Kanga ilobenuliwa, akh! hivi naitwa nani?
Kanga yanipagawisha, yanikosesha amani
Kanga wakijivalisha , napayukwa hadharani
Kanga yanipa mkesha, akivaa wa pembeni
Kanga inavyonikosha, naweza honga milioni
Kanga ya kifuani , pumzi nusu hupotea
Kanga ya kiunoni, huishia kuzimia
Kanga hizi si utani, asifiwe alovumbua
Kanga akiwa chumbani, burudani yatulia.
By Klorokwini a.k.a kibaka mzoefu
ningekuwa hivi wangenikoma
Umenifurahisha sana wafa kuwa mama mkwe
Kweli nimeamini Utu uzima dawaaaaaaaaaaaaaaaa!!!Ukiteka kipande cha nchi, shurti upandishe bendera!
Mwanakijiji kweli we ni mtata, maana duh! ila ndo wazee mlobakia cku hizi.
Kanga zina mambo mengi, zina mengi hizo kanga,
Kanga zinaficha vingi, vinavyofichwa na kanga,
Kanga zina siri nyingi, zina siri hizo kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!
Kanga zinaona mengi, chumbani ziliko kanga,
Kanga zahifadhi vingi, vyasitiriwa na kanga,
Kanga zafunika mengi, visivyoonwa bila kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!
Kanga zinagusa vingi vinavyoguswa na kanga,
Kanga zapangusa pengi, papanguswapo na kanga,
Kanga zina hisa nyingi, za wadau wenye kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga
Kanga zinaganda vingi, visivyoganduka bila kanga,
Kanga zinashinda nyingi, kweli vitenge si kanga,
Kanga zina rangi nyingi, na misemo kwenye kanga,
Kanga unapoachiwa , ana penzi mwenye kanga.
Kanga hata kama nyingi, atakupa moja kanga,
Kanga itasema mengi, kubwa ni hilo la kanga,
Kanga yatangaza vingi, hakuna kuzidi kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga.
UKIMPENDA ITUNZE.
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
(picha kutoka Mombasa Events)
nimependa shairi,kanga na mvaaji mwenyewe
sikujua zinamaana kiiiiiiivyo,
kumbe kuna haja yakuacha japo kipande kila unakopitia

Hivi haya kama siyo kunitia majaribuni ni nini sasa????????????
Nadhani mwenzetu unatafuta tu kisingizio cha kuingia majaribuni.
He!! Vipi kwani........hupendi kanga inavyopewa sifa??Na nyie mkome na mananiiii yenu yacyo na hekima. Mbna magaguro na vipens vyenu vyenye mabao kibao amviweki hadharan. Hamna lolote mmekosa 2 pa kutuliza hyo michebwengo yenu. Mwatiana hashki 2.
Nani zaidi kati ya 'Khanga moko ndembendembe - lakhi si pesa' na 'Kitu T'?
nimependa shairi,kanga na mvaaji mwenyewe
sikujua zinamaana kiiiiiiivyo,
kumbe kuna haja yakuacha japo kipande kila unakopitia