Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Angikana Tanzania pamoja na Askofu Jackson Sostenes wa Dayosisi ya Dar es Salaam, wamewasilisha pingamizi Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, wakipinga mashahidi watano akiwemo aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa, wasitoe ushahidi katika kesi ya ardhi iliyofunguliwa na Bernardo Sepeku.
Mbali na Mokiwa, mashahidi wengine wanaopingwa na kanisa hilo wasitoe ushahidi wao ni askofu wa Oscar Mnung’a wa Dayosisi ya Newala na John Mwamazi ambaye ni mchungaji mstaafu wa kanisa la Anglikana Dar es Salaam.
Wengine ni Blandina Sepeku (74), ambaye ni dada yake mkubwa na Bernardo pamoja na Abdallah Mtema ambaye ni mlinzi katika shamba lenye ukubwa wa ekari 20 lililopo Buza.
Bernado, ambaye ni mtoto wa marehemu John Sepeku aliyekuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Dar es Salaam, alifungua kesi hiyo ya ardhi namba 378/2023, akipinga kunyang’anywa zawadi ya kiwanja alichopewa baba yake mwaka 1978 na kanisa hilo.
Mtoto huyo alifungua kesi dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Kanisa Anglikana Tanzania, Askofu Jackson Sostenes wa Dayosisi ya Dar es Salaam na pamoja na Kampuni ya Xinrong Plastic Waste Industry Co Ltd.
Katika kesi hiyo, Bernardo anadai alipwe Sh3.72 bilioni ambayo ni fidia ya hasara ya kifedha iliyopatikana kutokana na uvamizi wa mali ya ardhi katika kiwanja hicho.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.