Kanisa Katoliki kujadili ombi msamaha wa Sitta

Kanisa Katoliki kujadili ombi msamaha wa Sitta

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712

Lowassa--Novermber3-2014.jpg

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana,Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.(Picha:Maabara)

Kanisa Katoliki Tanzania, limesema uamuzi wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kuliomba radhi Kanisa hilo kufuatia migongano iliyojitokeza kati ya viongozi wa serikali na wa Bunge Maalum la Katiba (BMK), ni jambo linalojadilika.


Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, alisema pamoja na uamuzi huo wa busara aliouchukua Lowassa, jambo hilo ni la hekima na kama litajitokeza katika mkutano ujao wa Baraza hilo utakaofanyika kesho litajadiliwa na kutolewa maoni ya pamoja ya Baraza.

"Ninakaa na wenzangu wa Baraza la Maaskofu, Novemba 4,mwaka huu (kesho), nalisubiri kama suala hilo la msamaha kama litakuja kwenye sura kama hiyo, tutalijadili na tutatoa maoni ya pamoja ya Baraza," alisema Askofu

Ngalalekumtwa na kuongeza: Alisema kama huyo aliyeambiwa (Askofu wa Mahenge) atalileta kama ajenda tutalijadili."

Askofu Ngalalekumtwa alisema mtu mmoja hawezi kutoa tamko hadi wakae kama Baraza kutoa maoni ya pamoja.

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli, aliomba msamaha huo wakati akitoa salamu zake katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge, mkoani Morogoro wiki iliyopita. Alisema Kanisa Katoliki lina mchango mkubwa katika kudumisha amani na mshikamano nchini, hivyo mambo yaliyojitokeza yanapaswa kusamehewa.

"Najua hivi karibuni tumewaudhi, lakini mimi naomba mtusamehe bure tu, kama vile mzazi anavyomsamehe mtoto wake anapokosea," alisema Lowassa na kuongeza kuwa Kanisa Katoliki ni muhimu katika maendeleo ya nchi.

Ingawa Lowassa hakueleza kwa undani tofauti zilizojitokeza kati ya Kanisa hilo na baadhi ya viongozi wa serikali, lakini wakati BMK likiendelea, taasisi za dini zilisambaza waraka uliosainiwa na viongozi wake ukilikosoa Bunge hilo kwa mambo mbalimbali ikiwamo kuendelea kujadili rasimu bila maridhiano kutokana na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia.

Kadhalika, viongozi wa madhahebu hayo ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT) na Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), walilikosoa BMK kwa kupuuza maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Waraka huo ulisababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kujiweka katika wakati mgumu kwa kuzua mgogoro dhidi ya viongozi wa dini ya Kikristo, baada ya kuita waraka huo kuwa ni wa kipuuzi na wa ovyo ovyo.

Sitta ambaye alitoa kauli hiyo Oktoba Mosi mwaka huu, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa waraka wa maaskofu una lugha ya Ukawa, ingawa maaskofu kwa upande wao waliueleza kuwa ni waraka wa kinabii, kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.

Sitta alitoa kauli ya kuuponda waraka huo bungeni alipokuwa akielezea mwenendo wa upigaji kura za kupitisha ibara na sura za rasimu ya katiba iliyopendekezwa kabla ya upigaji wa kura na wakati wa kutangaza matokeo, akisema watu wa Mungu kama maaskofu hawawezi kutoa waraka kama huo na kudai kuwa amekuwa akituhumiwa kwenye mitandao kwamba anadharau maaskofu.

"Nimalizie na viongozi wangu wa kiroho…mababa zangu maaskofu, natuhumiwa sana kwenye mablog kwamba nadharau maaskofu. Wakiwa na matendo kama hayo hao baadhi ya maaskofu itabidi tuendelee kuwadharau," alisema na kuongeza: "Ninao waraka huu ambao umelazimishwa kutumwa katika makanisa. Sioni utukufu wa Ukristo katika waraka huo. Huu waraka unamwamuru Rais airudishe Tume ya Mabadiliko ya Katiba."

Kuna Ukristo hapa?" Alihoji na kuendelea: "Waraka huu unamlazimisha Rais asitishe mchakato wa Bunge Maalum…tangu lini watu wa kiroho wanatoa maagizo ya kisiasa? Hii siyo haki hata kidogo…kuna Ukristo hapa? Waraka una lugha za wale Ukawa tuliowazoea."

"Hivi kweli maaskofu wa Kikristo wanaweza kusema kwamba Wizara ya Katiba na Sheria irudishe tovuti ya Tume ya Jaji Warioba na kuirejeshea nyaraka zake zote ili wananchi wasome na kujifunza?" alihoji Sitta.

"Kwamba maoni ya wananchi hayawezi kufutwa na kudharauriwa na chama tawala, hivyo basi Bunge la Katiba lijadili na kuboresha tu rasimu ya katiba na si kubadilisha," alisema Sitta.

"Waraka huu kwa shinikizo la maaskofu umesambazwa kwenye makanisa na kusomwa. Mimi nasema kama Mkristo, tukianza kuruhusu nchi yetu kutoa nyaraka hizi za kisiasa zisomwe makanisani kwa kudai huo ni msimamo wa maaskofu, basi nchi hii tutaipeleka kubaya. "Na mini kama mtu mzima lazima nionye kuhusu tabia hii, ukizingatia nchi hii haina dini, hawa baadhi ya maaskofu ambao walikusanywa Dar es Salaam na makundi yale yale yanayohusishwa na Ukawa, kama wao ni wanachama wa siri wa vyama vya siasa vinavyochukia CCM wajitokeze waziwazi," alisema Sitta.

Sitta aliendelea kunukuu waraka huo kwamba kuna askofu mmoja ameapa kwamba atawaelimisha waumini wake ili siku za usoni wawashughulikie viongozi kama mimi (Sitta). Nasema aendelee, lakini Mungu anaona yote yaliyo moyoni mwetu." Baada ya Sitta kutoa kauli hiyo, Askofu wa Jimbo la Katoliki la Bunda, Mhashamu Renatus Nkwande, alisema matamshi ya Sitta yanaonyesha anavyohangaika kualalisha kilicho haramu.

Alisema kitendo cha Sitta kuendesha BMK kwa kukejeli wajumbe wenzake walioondoka bungeni (Ukawa) na wajumbe walioandaa rasimu ya pili kwenye Tume ya Katiba Mpya chini ya Jaji Joseph Warioba, ni jambo la aibu ambalo halivumiliki, na ndiyo maana walitoa waraka wa kutokubaliana nacho. "Kwa kweli Sitta ametutukana, ametafuta ubaya kwa viongozi wa dini, kwa kuwa tumesema ukweli ? Sisi tulikuwa tunatimiza wajibu wetu kwa Wakristo …tulizungumza kutokana na hitaji la wakati, na ulikuwa waraka wa unabii," alisema.

Viongozi wengine wa kanisa Katoliki waliojibu kauli za Sitta ni Makamu Mwenyekiti wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Dk. Methodius Kilaini, ambaye alinukuliwa akisema kuwa Sitta amelewa madaraka.

Wakati hayo yakiendelea, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Anthony Komu, amesema viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Sitta ndio waliopaswa kuliomba msamaha Kanisa.

Akizungumza katika mikutano iliyofanyika Kata za Mabogini, Kibosho Magharibi na Kibosho Kirima, Jimbo la Moshi Vijijini kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali za serikali za mitaa, Komu alisema:

"Unawezaje kuwaombea msamaha watu ambao hawajui kama wamefanya kosa.

"Angeishauri CCM na serikali yake imwambie Sitta ajutie kosa lake kwa kuwakebehi viongozi wa dini waliotoa mawazo yao kuhusu kupuuzwa kwa maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba."

CHANZO: NIPASHE
 
nipashe wanapenda sana mipasho jamani

Hakika dada. Hawa Nipashe, ITV na Radio One ni vyombo vya habari ambavi vipo kimipasho kwa lengo la kumjenga mtu fulani na kumbomoa mwingine
 
Tafadhali kanisa Sitta ni mnafiki mkubwa mmeshuhudia jana kuajiri vijana kumpiga waziri mkuu mstaafu Warioba,chonde chonde mtengeni Sitta kabisa ni muuaji na hata koma tabia zake
 
nimesikia na kusoma katika vyombo vya habari edward lowassa akihutubia katika maadhimisho ya miaka 50 ya jimbo katoliki la morogoro akiliomba kanisa katoliki radhi kutokana na matusi yaliyoelekezwa kwa maaskofu wa cct wakiwemo wa kanisa hilo na mwenyekiti wa lililokuwa bunge maaalumu la katiba aliyewaita maaskfu hao mashetani. ninavyojua mimi mtu akikosa ni lazima kwanza aone uchungu na chukizo kwa kosa lakie kisha yeye mwenyewe aamue kuomba radhi/msamaha ili asamehewe. sijaelewa ni nini hasa kimemsukuma lowassa kujitwika zigo la kutubia na kuomba msamaha kwa ajili ya dha,bi na udhalilishaji mkubwa aliofanya samwel sita(hasimu wake wa kisiasa) ilihali sitta mwenyewe ameridhika kwa kile alichowatamkia maskofu.hivi kama lowassa aliguswa na matusi yale kwanini hakuyakemea kipindi kilekile kama alivyokemea tatizo la ajira kwa vijana?
nawasilisha.
 
Matusi aliyotukana Sitta dhidi ya viongozi wa dini yatamtafuna milele..

Sitta ni laana katika nchi..
 
Anayepaswa kuomba msamaha ni Sitta mwenyewe na si Lowassa kama kweli anajutia aliyoyaongea!!
Hapa mnatakiwa kuelewa kuwa EL kwa namna fulani anataka kufufua mjadala kwamba kuna kosa fulani alilifanya hasimu wake kisiasa yaani SS. Lengo hasa la EL sio kuomba msamaha, lengo ni kusambaza awareness ya kosa lililofanywa na Six
 
Hapa mnatakiwa kuelewa kuwa EL kwa namna fulani anataka kufufua mjadala kwamba kuna kosa fulani alilifanya hasimu wake kisiasa yaani SS. Lengo hasa la EL sio kuomba msamaha, lengo ni kusambaza awareness ya kosa lililofanywa na Six
Hahahahahahaahhaa Jabulani hayo ni maoni yako
 
kwani Lowasa aliomba msamaha kwa kosa gani lililofanywa na serikali?

Inahitaji akili pana na kupitia malezi ya kiungwana ili kugundua kosa au utovu wa nidhamu. Sishangai kuona kwamba hukuliona kosa kwenye jambo hili, na hukuona sababu ya kuomba radhi.
Sikulaumu kwa sababu ndio uwezo wako ulikoishia na huna cha ziada cha kukuvusha zaidi ya hapo kutokana na kile nilichokieleza hapo juu.
Ova
 
Sitta ni mjinga sana kama kweli alikuwa na nia ya kugombea urais basi asingepaswa kutoa kauli mbovu kiasi kile wenzake sasa wanatumia nafasi hiyo kummaliza kabisa.
 
Hapa mnatakiwa kuelewa kuwa EL kwa namna fulani anataka kufufua mjadala kwamba kuna kosa fulani alilifanya hasimu wake kisiasa yaani SS. Lengo hasa la EL sio kuomba msamaha, lengo ni kusambaza awareness ya kosa lililofanywa na Six

kaka. that smartness you have doesn't match the cerebral capacity of most of members here.
ulichokisema ndicho kilicho sahihi 100% tatizo ni kwamba, huu msusruru wa wajinga humu wana uwezo wa kujua hilo!!!
 
Asante sana Lowassa kwa kuisaidia serikali, wewe ni jasiri na shupavu wa hali ya juu
 
Busara ya upendo
Hakuna cha busara mkuu, kama hakupendezwa na ile hali kwann akuinyesha wakati uleule kwa kupinga yale maneno? Sion maaskofu wanachoenda kujadir sababu nikose mm uje kuomba radhi ww inakujaje? Ni yesu aliebeba dhambi za wengine na hakuna mwengine dunia atakaefanya hvo (kila mtu atabeba msalaba wake)
 
Back
Top Bottom