[h=6]Kanisa Katoliki lahoji
madaraka ya Rais
LATOA MWONGOZO WA MAONI YA KATIBA, LATAKA ASITEUE MAJAJI, WABUNGE WAKUU
WA MIKOA, ASHTAKIWE
KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limetoa mwongozo kwa waumini
wake, likiwataka kushiriki mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya, huku
likihoji madaraka makubwa aliyonayo Rais katika mambo
mbalimbali.[/h]
Hongereni maaskofu! Haya... tusubiri miongozo ya viongozi wa Wasukuma, Waha, Freemansons, Salafi, nk. kwa wanachama wa jumuiya zao
Ndiko tunakoelekea huko! Natamani kusikia muongozo toka kwa wazee wa Kikurya huko Tarime. Nadhani wao watatoa muongozo kwamba musuba uhalalishwe ndani ya katiba na kuwa zao la biashara.
wasukuma watataka chagulaga iwe halali kikatiba.
Kwa hiyo wakatoliki tutatoa maoni kama kundi baada ya kupata mwongozo toka kwa maaskofu? Vitu kama hivi ndivyo huleta chokochoko. Wenzetu wa upande wa pili nao wakitoa muongozo kwamba mahakama ya kadhi iingie kwenye katiba itakuwaje?
Najua maaskofu wameongelea tu hayo madaraka ya rais lakini hivi ni muhimu wao kutoa muongozo kwa waamini? Kwa nini tusiachiwe tutoe maoni yetu kama watu huru bila viongozi wetu wa kiroho kuingilia? Hayo yatakuwa ni maoni ya kanisa au maoni ya waamini?
Ndiko tunakoelekea huko! Natamani kusikia muongozo toka kwa wazee wa Kikurya huko Tarime. Nadhani wao watatoa muongozo kwamba musuba uhalalishwe ndani ya katiba na kuwa zao la biashara.
wasukuma watataka chagulaga iwe halali kikatiba.
Muda si mrefu utasikia wale jamaa nao wanatoa mwongozo. Yangu macho na masikio.
Unamaanisha nini unaposema kanisa katoriki limetoa mwongozo?weka ushahidi tuone kama ni MWONGOZO au NIMAONI? weka nakara tusome wenyewe.[h=6]Kanisa Katoliki lahoji madaraka ya Rais LATOA MWONGOZO WA MAONI YA KATIBA, LATAKA ASITEUE MAJAJI, WABUNGE WAKUU WA MIKOA, ASHTAKIWE KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limetoa mwongozo kwa waumini wake, likiwataka kushiriki mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya, huku likihoji madaraka makubwa aliyonayo Rais katika mambo mbalimbali.[/h]