Kanisa Katoliki lisiogope kumtafuta Emmanuel Nchimbi. Kwa hadhi ya Nchimbi sio ya kuacha apotezwe

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
29,314
Reaction score
93,919
Nafahamu ni wengi nchini wanatekwa, wanauliwa. Nafahamu katika mizani ya kiroho, binadamu tu sawa.
Kuna vijana wametekwa sababu ya mapenzi. Jukumu la Kanisa ni kusemea sauti za vijana hawa.

Kwa Nchimbi, ni tofauti kabisa. Huyu hata Mbinguni anatambulika kwa nafasi zake za kisiasa. Hakuwa tu muumini, huyu alikuwa muumini Mkatoliki namba mbili katika mizani ya Serikali. Hakuiba mke wa mtu, hakudhulumu mali.

Ametekwa sababu ya kusema, "Tupambanie tupate Katiba."

Kutekwa kwake kunaibua wazee kama akina Wasira na kuanza kuongea upuuzi na ujinga mwingi, watoto kama akina Kawaida kumtusi Nchimbi. Kana kwamba kwao suala la kumteka Nchimbi ni suala dogo kabisa. Sasa kama anafanyiwa hivyo Nchimbi, ni vipi kuhusu mwananchi wa kawaida?

Wananchi wanataka kumsikia na kumuona Nchimbi ili wawe na amani.

Waumini wanataka kumuona Nchimbi ili wawe na amani.

Kanisa halitakiwi kuogopa kumtafuta Nchimbi kwa kuhofia kile kinachoitwa "mgogoro wa kidini".

BAKWATA ni kundi la kihuni, ni wahuni wanaofanya kazi kwa maelekezo. Msione wanaita vyombo vya habari na kuanza kutishia tishia. BAKWATA haina ushawishi wowote kwa raia wa Tanganyika.

Kanisa lisiogope kumtafuta Nchimbi. CCM mahali ilipofikia imechokwa na Watanzania wote, si Waislamu, si Wakristo. Habari njema ni kwamba, yeyote anayesimama kupinga uovu wa CCM, basi Watanganyika wote, Waislamu na Wakristo, humuunga mkono.

Nitoke rai yangu!

Nchimbi mpaka anatekwa alikuwa ni Mkatoliki namba moja katika mizani ya Serikali, ambayo kwake alikuwa raia namba mbili!!
 
ok.🐒
 
Kwanza naunga mkono hoja, ikitokea kuna muumini wa dhehebu fulani haonekani ibadan, viongozi wa kanisa husika wana haki ya kumtembelea muumini wao,

Kwa vile Nchimbi ni Mkatoliki akisali parokia ya St. Peter's, baada ya kuhama pale, atakuwa anasali kule alikohamia, hivyo bado ametulia, ataripoti Jumuiya yake mpya na kushiriki ibada. https://www.jamiiforums.com/threads...ikiliwa-ni-ameamua-kutulia-kunyamaza.2469446/
P
 
Tec na kanisa hali mtafuti mtu wala halimfukuzi mtu na pia kama bado yupo na imani ya rc basi jumuiya yake ndio inaweza kumulizia mwanajumuiya wenzie na sio kanisa lakini pia hata jumuiya haina nguvu kumtafuta maana haina vyombo hapo mwenyekiti wake wa mtaa,mtendaji wa mtaa wake na ofisi yake ya zaman ndio zenye mamlaka
 
Hakuna mwenye akili timamu anaweza kusikiliza "rants" zako za kijinga na kipumbavu!
 
Kanisa lisibebeshwe mzigo wa kumtafuta Nchimbi,ni sawasawa na kusema suala la Nchimbi aachiwe Mungu.
Kama wananchi wana wasiwasi juu ya kiongozi wao kuto kujua mahali alipo wamechukua hatua gani dhidi ya serikali ?
Kama wapo waprotenstanti, waislamu,wapentekosti na wasio na dini wanao uumia kwa kuto muona kiongozi "kipenzi" chao,iweje wasichukue hatua ya kumtafuta "nyumba kwa nyumba" hadi walio mficha wamtoe waliko mficha kabla ya "hasira za damu" za watafutaji na wafichaji hazija fikia kipimo cha liwalo na liwe?
Watanzania tuache kulalamika hovyo na kila lililo tofauti na matakwa yetu kumuachia Mungu ndiye alitatue.
Twende kati kwa umoja wetu, nyumba kwa nyumba, mkoa kwa mkoa,shimo kwa shimo....
Wote watapatikana iwe mifupa au nyama mbichi,hata ikivunda muhimu watakuwa wamepatikana.
 
Naunga hoja mkono
 
Acha kuleta mizaha kwenye mambo ya uhai wa mtu kiroho na kimwili..! huwa unafikiri lkn mizaha yako ina gharama gani kwa familia yako..watoto wako km wapo..? au wewe ni msela huna wajibu kifamilia, km ni hivyo sawa endelea na mizaha yako..lkn Mungu hapendi mizaha!
 
Waumini wakatoliki ni wa ajabu sana, ni Mababa Askofu tu ndio wanaijua na kuitekeleza imani ya kanisa katoliki..waumini ni wanafiki, ni waumini wa sherehe na matamasha tu, ukristo sio matamasha na sherehe..unashindwa kumtetea jirani na muumini mwenzio km nchimbi unayemjua na kumuona..UTAWEZAJE KUMTETEA KRISTO AMBAYE HUMJUI NA HUJAWAHI KUMUONA? Naomba mjibu waumini wakatoliki!
 

Asante sana mkuu niliwahi kuandika Uzi kama huu
 
Yupo salama huyu mh ni vile kazi yake aliyoilia kiapo imemtaka kukaa kimya tu.
 
Sura yake na matendo yake haviendani.
Jiulize kwanini shetani alianza kumdanganya kwanza HAWA kule peponi na sio Adam mwenyewe?
Hichi kumbe ni katili sana kama aliweza kuongea hata na shetani.japo ni mama zetu.
Angekuwa ni mwanaume wangeshayamaliza na kuendelea na maisha ila hawa mama zetu wanakaa na vinyongo
 
CCM watuambue alipo Nchimbi.
Huyu ni Makamu wa Rais, ni Public figure.
Anaachiaje madaraka bila kukabidhi ofisi?
Yaani Raia namba 2 nchini, wanakuja na majibu mepesi tu eti hawajui alipo!
Waache kuleta mizaha katika mambo ambayo ni serious.
 
Sasa kanisa limtafute nchimbi kama nani kwao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…