Kanisa Katoliki mnataka kutuharibia nchi?

Kila ikifika jumapili huwa nakua na mzuka sana wa kwenda kanisani ila nikifikiria kinachoendelea huwa naona bora nifanye ishu zingine,sio walokole,walutheran wala wasabato wote lao moja tu mniache[emoji124]
 
Ibada msikitini, kwa mzee wa bapa, kkkt nk na hukobkote viongozi wakisali wanahutubia na kutoa misimamo ya serikali, We umeona Katoliki tu? Sisi tunasubiri kuletewa mabango kitita tutekeleze ishu ya imesemwa wapi haijalishi mradi aliyesema ni mtu sahihi.
 
Soon naachana na roman bora niwe mpaganu
 
Kwamba hujui chochote kuhusu C.atholic C.hurch M.ovement au
 
Unataka nchi iharibike mara ngapi! Viongozi wa dini ni wachumia tumbo tu hawana lolote. Ni wasabato pekee ndio hawaruhusu ujinga huo makanisani kwao kwa sababu hawategemei misaada ya serikali na wanasiasa kuendesha mambo yao
Ila wasabato kweli wako vizuri. Sijaona wakijikomba kwa wanasiasa na huwezi kuta wanasiasa wanaingia kwenye makanisa yao kutoa hotuba za kisiasa. Mwanasiasa ukimpa jukwaa lazima alitumie kisiasa
 
Kwamba hujui chochote kuhusu C.atholic C.hurch M.ovement au
Hii sifahamu kama hapa kwetu pia imeanza japo baadhi ya nchi imeanza tayari.
 
Maneno yako sawia maana haya yangefanyika misikitini ingekuwa kelele sana ni vyema nyumba za ibada zikawekwa mbali na siasa
Na yamefanyika kanisani si ndo kelele hizi..!?
 
Dini na Siasa ni wale wale (kitu kimoja)

ni sawa sawa na wacheza kamali na vibaka

Mcheza kamali ndiye kibaka na Kibaka ndiye Mcheza kamali

Mchana Kibaka hucheza kamali, Usiku kibaka huyo huyo hukaba watu
 
Mwadhama Cardinal Polycarp Pengo.

Uliza Wakatoliki juu ya hicho cheo watakuelekeza wadhifa alionao Cardinal Pengo.
Sasa mimi ni Mkatoliki..Nakuambia hivi Pengo ni Askofu Mkuu wa Metropolitan ya Dar es Salaam tu....

Tz kuna Metropolitan 6 ...Zote zina maaskofu wakuu ambao wapo Answerable to Pope moja kwa moja..
 
Kanisa halipo kwa ajili ya kuridhia utashi wako! Kwa sababu tu hujasikia unachokitaka ndio kanisa liharibu nchi? Umekosa utii, nenda katubu
 
Sasa mimi ni Mkatoliki..Nakuambia hivi Pengo ni Askofu Mkuu wa Metropolitan ya Dar es Salaam tu....

Tz kuna Metropolitan 6 ...Zote zina maaskofu wakuu ambao wapo Answerable to Pope moja kwa moja..
Kuna wakati Kilaini alikuwa Jimbo Kuu la Dar es salaam. Je nani alikuwa boss wake?

Anyway tuachane na habari ya vyeo tujikite kwenye hoja ya msingi.
 
Kanisa halipo kwa ajili ya kuridhia utashi wako! Kwa sababu tu hujasikia unachokitaka ndio kanisa liharibu nchi? Umekosa utii, nenda katubu
Umewahi kuona mtu anatubu kwa kusema ukweli?
 
Kuna wakati Kilaini alikuwa Jimbo Kuu la Dar es salaam. Je nani alikuwa boss wake?
Umeshasema alikuwa Jimbo la Dar....Kama alikuwa jimbo la Dar basi alikuwa chini ya Metropolitan ya Dar yenye Askofu mkuu Pengo...

Anyway tuachane na habari ya vyeo tujikite kwenye hoja ya msingi.
Ni vyema mambo msiyoyajua wuwe mnaomba ufafanuzi kutoka kwa wanaofahamu
 
Nakubaliana na wewe.. Na hili sio kwa kanisa katoliki tu..

Viongozi wote wa kidini wamejisahau sana..

Hakuna jambo baya kama kuruhusu kanisa la Mungu kuwa sehemu ya viongozi wa kisiasa kuzungumzia utendaji wao.

Sitaki kuwalaumu hao viongozi wa kisiasa kwa sababu hawaziombi hizo nafasi bali ni viongozi wa kanisa ndio wanawatetemekea na kuwapa mwanya mkubwa wa kusema!!

Ifike sehemu hata mkuu wa nchi akihudhuria ibada aende kama muumini wa kawaida tu na wala asikubali kusema chochote katikati ya ibada..

Watu wanapokwenda ibadani wote ni sawa na kiongozi wao ni yule anayeongoza ibada..

Viongozi wa nyumba za ibada waache kuwatetemekea viongozi wa kisiasa!
 
Hili kanisa ni sinagogi la yule aliyehubiriwa enzi na enzi ambae hatutauza wala kununua bila chapa ...kama lilikaa kimya na kubariki biashara ya utumwa kwa jina la YESU wategemea nini ktk karne hii????????????????
 
Umeshasema alikuwa Jimbo la Dar....Kama alikuwa jimbo la Dar basi alikuwa chini ya Metropolitan ya Dar yenye Askofu mkuu Pengo...

Ni vyema mambo msiyoyajua wuwe mnaomba ufafanuzi kutoka kwa wanaofahamu
Umeshinda, jikite kwenye Main Topic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…