kiLimIlire
JF-Expert Member
- Apr 8, 2012
- 389
- 884
Habari wana JF, naomba kuongezewa uelewa juu ya mambo ya Hisa na namna ambavyo mtu anaweza kushawishika kununua na kuuza hisa, nikizingatia mchakato wa ununuzi wa hisa ulioendeshwa na Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki nchini Tanzania.
Baada ya kuwashawishi waumini walio wengi kufikia maamuzi ya kununua hisa za kawaida za benki hiyo kwa bei 'rahisi', wakiaminishwa kuwa pesa wanayonunulia hisa hizo itakuwa ikiongezeka maradufu kila mwaka, mambo yamekwenda kinyume na matarajio ya wanunuzi wa hisa hizo kwani, ni takriban miaka sita tangu 'mradi ' huo uanze na bado watu hao hawawezi kuvuna chochote.
Taarifa kutoka kwa uongozi wa benki hiyo ni kuwa wateja hao hawawezi kuchukua kilicho chao kwa kuwa bado mtaji wa benki hiyo bado ni mdogo, pia hawajajiunga na soko la hisa la Dar es Salaam hivyo hakuna uwezekano wa wanunuzi wa hisa zao kujitoa katika biashara ya hisa za Mkombozi hadi hapo taarifa itakapotolewa.
Naomba kujuzwa
1.Katika misingi ya biashara za hisa, hiyo hali ni ya kawaida
2.Je mbona hakuna taarifa wazi juu ya trend ya biashara hiyo inayomwezesha mteja wao kufanya maamuzi. Iwapo aendelee nao au ajitoe
3.Je iwapo mteja wao akifariki na warithi wakataka pesa ya mzazi wao, hazichukuliki.
Msaada tafadhari ili niondokane na dhana ya utapeli dhidi ya Benki ya Mkombozi.