Kanisa Katoliki na Hisa za Kawaida za MKOMBOZI BANK, kuna UTAPELI

kiLimIlire

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2012
Posts
389
Reaction score
884
Habari wana JF, naomba kuongezewa uelewa juu ya mambo ya Hisa na namna ambavyo mtu anaweza kushawishika kununua na kuuza hisa, nikizingatia mchakato wa ununuzi wa hisa ulioendeshwa na Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki nchini Tanzania.

Baada ya kuwashawishi waumini walio wengi kufikia maamuzi ya kununua hisa za kawaida za benki hiyo kwa bei 'rahisi', wakiaminishwa kuwa pesa wanayonunulia hisa hizo itakuwa ikiongezeka maradufu kila mwaka, mambo yamekwenda kinyume na matarajio ya wanunuzi wa hisa hizo kwani, ni takriban miaka sita tangu 'mradi ' huo uanze na bado watu hao hawawezi kuvuna chochote.

Taarifa kutoka kwa uongozi wa benki hiyo ni kuwa wateja hao hawawezi kuchukua kilicho chao kwa kuwa bado mtaji wa benki hiyo bado ni mdogo, pia hawajajiunga na soko la hisa la Dar es Salaam hivyo hakuna uwezekano wa wanunuzi wa hisa zao kujitoa katika biashara ya hisa za Mkombozi hadi hapo taarifa itakapotolewa.
Naomba kujuzwa
1.Katika misingi ya biashara za hisa, hiyo hali ni ya kawaida
2.Je mbona hakuna taarifa wazi juu ya trend ya biashara hiyo inayomwezesha mteja wao kufanya maamuzi. Iwapo aendelee nao au ajitoe
3.Je iwapo mteja wao akifariki na warithi wakataka pesa ya mzazi wao, hazichukuliki.
Msaada tafadhari ili niondokane na dhana ya utapeli dhidi ya Benki ya Mkombozi.
 
Ilo ni somo refu sana, kwa mtu layman in investments and business management itachukua siku nzima.Hakuna utapeli ila ni uelewa tu.Mjini kuna maconsultant wa business jaribuni kuwa mnaonana nao kabla ya kufanya investments.au nipm ni kujulishe kwanza by consultancy fee kidogo.
 
Kuna kitabu kimeandikwa na mtanzania kinaelezea juu ya haya mambo ya hisa na uwekezaji tafuta bookshop iliyokaribu kinunue ujisomee utaelewa uzuri wa kitabu chenyewe kimeandikwa kwa kiswahili.

Natumaini nitakuwa nimekusaidia.
 
Kwa hiyo kanisa lili-take advantage ya u-layman wa waumini na kuwaingiza katika mambo ya kitaalam si ndo utapeli wenyewe huo
 
Katiba yaoinaelezea vipi kuhusu kujitoa? maana hawa jamaa hawapo sokoni useme kama utauza hisa.
 
Aisee nami nilimnunulia mwanangu hisa ka 500 hivi, lakini sijui kinachoendelea.
 
Aisee nami nilimnunulia mwanangu hisa ka 500 hivi, lakini sijui kinachoendelea.

ni mambo ya ajabu kabisa, nenda benki uone majibu utakayopewa, nalipenda kanisa langu lakini kwa majibu nilyopewa nilikuwa totaly dissapointed... wanakatisha tamaa
 
pamoja na uelewa wako mdogo nadhani umeshauliwa vema kwamba tafuta consultant watakusaidia pia fuatilia magazeti sheria ya Tanzania inayataka mabenki yote kutoa STATEMENT OF AFFAIRS/financial statement kila baada ya miwezi mitatu kwa mwaka mara nne,hapo unaweza kujua kama benki yako inaendeshwa kwa hasara au faida.Nakama kuna wasiwasi benki kuu ndio wenye dhamana,fanya utafiti ulidhishe nafsi yako usitegemee sana maneno ya mitaani.
 
Kanisa Katoliki ni kubwa sana duniani. Benki Mkombozi ni moja ya miradi ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam (siyo miradi ya kanisa katoliki nchi nzima). Sasa kulitaja kanisa Katoliki sijui ulimaanisha nini, kwa maana usishangae hapo pembeni tu Jimbo la Sumbawanga wakawa hawaijui kabisa hiyo benki. Ni vyema title ya thread yako inge.base kwenye Mkombozi Bank.

Au utendaji wa Bank M ukiwa mbovu huwa analalamikiwa Nimrod Mkono? Utendaji wa NBC ukiwa mbovu huwa tunakimbilia kumlalamikia kaburu? Hapana, unaanza ngazi ya branch, anza pale maulizo, usiporidhika unawaomba uonane na meneja. Mara chache sana huwa tusiporidhishwa na meneja huwa tunaenda HQ.

Inawezekana pia umelitaja kanisa Katoliki labda pengine (sina uhakika) mlitangaziwa kanisani, lakini bado inabaki kwamba tangazo la pale ni kama tangazo la ITV au TBC, sio tangazo la Kanisa Katoliki (ukumbuke Kanisa Katoliki linafika hadi kwa Papa Francis). Hebu jaribu kumuona branch manager hapo, ukikosa majibu nenda HQ uulize mtu gani sahihi wa kujibu maswali yako, watakuelekeza. Huenda uliishia kwa mfanyakazi wa kawaida wa benk na ulipokosa jibu zuri ukaja JF
 

na unaamini consultancy ni kitu common kwa watanzania wa kawaida, binafsi nitakwenda kwa kuwa ndio ushauri niliovuna hapa JF.... lakini wakati mchakato wa kuziuza hisa hizo hawakueleza habari ya kuwa mteja akitaka kupata info zao basi atafute consultant, na bado wateja wake wengi si wa mjini tu bali hata huko vijijini wametapakaa tena bila kujua what next baada ya sintofahamu hii. Harufu ya utapeli haijafutika bado
 
Aisee nami nilimnunulia mwanangu hisa ka 500 hivi, lakini sijui kinachoendelea.

Ile pesa iliyohamishwa kutoka Tegeta Escrow account si ndo inagawiwa kupitia hiyo benki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…