Kanisa Katoliki Tanzania linaendelea kutimua vumbi katika sekta ya elimu ya juu!

Kanisa Katoliki Tanzania linaendelea kutimua vumbi katika sekta ya elimu ya juu!

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,878
Reaction score
5,432
Askofu mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo kuu la Arusha, Tanzania katika mahojiano maalum na Radio Vatican wakati huu Kanisa Katoliki nchini Tanzania linapoadhimisha Miaka 150 tangu Wamissionari wa kwanza walipotua Visiwani Zanzibar, huo ukawa ni mlango wa Imani kwa Kanisa Katoliki, linajivunia mchango wake katika sekta ya elimu nchini

Anasema, kwa hakika Kanisa limekuwa ni mdau mkuu wa maendeleo ya elimu nchini Tanzania kuanzia katika shule za awali, msingi, sekondari, vyuo na sasa linaendelea kucharuka katika mchakato wa maboresho ya elimu ya juu. Hii ni changamoto iliyotolewa na Mapadre, Watawa na Waamini waliokerwa na uduni wa elimu ya Tanzania kwa wakati huo, wakaamua kulivalia njuga tatizo hili kwa kuwekeza katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Tanzania, SAUT, leo hii, anasema Askofu mkuu Lebulu, kinatimua vumbi nchini Tanzania! Wengi walidhani kwamba, hii ilikuwa ni nguvu ya soda, lakini matunda yake yanaendelea kujionesha sehemu mbali mbali za Tanzania.

Alipohojiwa kuhusu "siri ya mafanikio haya" Askofu Mkuu Lebulu hakusita kusema kwamba, ni jeuri, ari na hamasa iliyotolewa na Mapadre pamoja na Watawa walioamua kwa dhati kabisa kuwekeza katika uongozi bora, wakitafuta mafao ya watanzania wengi; wakaonesha mipango na mikakati endelevu kwa ajili ya maboresho ya sekta ya elimu ya juu nchini Tanzania. Wakatafuta, wakakusanya na kuzalisha fedha kwa ajili ya ustawi wa elimu Tanzania. Fedha hii imetumika barabara na matokeo yake ni kuendelea kupanuka kwa SAUT sehemu mbali mbali za Tanzania!

Hawa ni Mapadre waliotambua na kudhamiria kuendesha sekta ya elimu chini ya uongozi na usimamizi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwa kuongoza kisayansi na hivyo kuingia katika ushindani wa soko la elimu ya juu kisayansi, wakiwa na lengo la kuwapatia watanzania wenzao elimu iliyo bora zaidi, itakayowasaidia kupambana na mazingira yao, ili Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, iwe ni mahali pazuri zaidi pa kuishi!

Askofu mkuu Josephat Lebulu anakiri kwamba, Kanisa Katoliki nchini Tanzania lilisinzia kidogo katika kuwekeza kwenye mfumo wa elimu ya juu, lakini baada ya kutambua umuhimu wake, leo hii linaendelea kutimua vumbi! SAUT, haishikiki!
 
Ongea kwa data. Hata waislam wakija kusema kama Askofu Lebullu watakua sawa.
 
SAUT inatimua vumbi kwa vyuo gani kwa mfano????
 
Madhehebu mengine yafuate mfano wa kanisa katoliki ili tupige hatua za maendeleo kwa haraka.
 
Hongera kanisa kwa kutambua umuhimu wa elimu ya juu na kuanzisha vyuo vikuu nadhani wengine nao waige mfano huu ili Tanzania isonge mbele na tuache kubeza kwa kuleta mambo ya udini hapa kwani wanasoma wote bila kujali imani ya mtu.Hongera kanisa kwa hatua hii.
 
(et!! na kiimani mmefanikiwa kiasi gani?)Alie na macho haambiwa tazama,ongeza uwezo wa kufikiri usiwe mfinyu wa tafakari!utapata majawabu yapo hai!!ndugu!
 
Kwasasa SAUT wanazidi kufungua matawi kwenye miji mikuu Mfano Hapa Arusha wameshafungua ambapo nasikia watachukua zaidi ya wanafunzi ya 10,000 kwa kuanzia...
SAUT inatimua vumbi kwa vyuo gani kwa mfano????
 
Na kiimani mmefanikiwa kiasi gani !?
Imefanikiwa kuwafanya watu wawe na upendo miongoni mwao. Kama hawa wangeachiwa wakajiunga na ile dini nyingine, bila shaka Tanzania ingekuwa na wauaji wengi sana
 
Bungando, SAUTI YENYEWE, IFAKARA, MTWARA, RUCO, TABORA ARCHBISHOP mihayo, songea, Arusha, Morogoro. Maeneo yote haya nilyotaja kunabranches za SAUTI. Hadi sasa wanavyuo zaidi ya kumi, nafikiri wanakimbizana tu serikali
 
Imefanikiwa kuwafanya watu wawe na upendo miongoni mwao. Kama hawa wangeachiwa wakajiunga na ile dini nyingine, bila shaka Tanzania ingekuwa na wauaji wengi sana

Vipi kuhusu ushoga na ndoa za jinsi moja na tabia za viongozi wa kikatoliki kiujumla haswa upande wa maadili !?
 
SAUT imekuwa sana ina matawi Bukoba,Tabora, Mtwara, Songea na Iringa na Arusha.
 
Vipi kuhusu ushoga na ndoa za jinsi moja na tabia za viongozi wa kikatoliki kiujumla haswa upande wa maadili !?
nitajie mashoga kumi wanaotajwa kwenye udaku hapa Bongo, halafu uangalie dini yao ni ipi. Chezea anti Abubacar wa Magomeni wewe!
 
Back
Top Bottom