Kanisa la kiboko ya wachawi limefungwa Rasmi

Kanisa la kiboko ya wachawi limefungwa Rasmi

stabilityman

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2024
Posts
259
Reaction score
483
Asanteeee serikali
KAULI NZITO YA ASKOFU BAADA YA SERIKALI KUFUNGA 'KANISA LA KIBOKO YA WACHAWI!

Ndugu Watanzania!
Leo ni Siku ya Dominika. Lakini ninapojiandaa na mimi kwenda 'kukomunika' pamoja na watu wengine wa Mungu kama ilivyo desturi yetu ya Wakristo kwa siku kama ya leo, nimewiwa sana niwaandikie ujumbe.

Tangu jana tarehe 27 Julai nimeletewa kipande cha barua inayosadikiwa kutoka katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ikionesha Serikali imelifunga Kanisa lijulikanalo kama Christian Life Church linaloongozwa na Mch. Dominique K. Dibwe maarufu kama Kiboko ya Wachawi. Sababu za kulifunga Kanisa hilo zimeelezwa ndani ya barua hiyo ikiwemo kutoza watu pesa kiasi cha shilingi 500,000 kumuona kiongozi.

Kwa upande wetu, suala sio kutoza kiasi hicho cha pesa kwani yapo Makanisa mengi ambayo hutoza kiasi cha pesa zaidi ya kiasi hicho lakini wao hutumia mbinu za ziada. Kwa mfano, kile kitendo cha kuwauzia waumini maji, vitambaa, mafuta, nk hizo pesa zikiwekwa pamoja kiasi kinachopatikana ni zaidi ya hiyo shilingi 'tenga tano' zinatozwa na Mch. Dominique Kibwe!

Kikubwa kinachotushangaza ni kwa kiwango gani Serikali ya Tanzania imesajili huduma za Waganga wa Kienyeji kwa mgongo wa Kanisa. Tuna wasiwasi mkubwa kuwa kuna rushwa ya usajili katika mifumo yetu ya usajili nchini kwa kuwa hawa jamaa pia husajili kwa urahisi sana makanisa yao wakati hawana hata elimu, vyeti na hata uzoefu wa huduma achilia mbali hata recommendations stahiki toka kwa watu walio stahiki. Pia, wengi wao hawajawahi kuhudhuria vyuo vya Biblia achilia mbali Shule au vyuo vya theologia.

Kinachotushangaza zaidi ni kuwa katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia, maombi ya usajili wa Makanisa ambayo viongozi wao ni watu wenye sifa, uzoefu na uwezo na hata pia katiba, miongozo na mafundisho yao viko sawa hafanyiwi kazi kirahisi lakini wahuni, matapeli, waganga na waaguzi hupewa usajili bila shida ye yote. Tuna mashaka pia kuwa serikali hutoa haraka usajili kwa watu hawa ili kusudi iweze kuwatumia kirahisi lakini kwa kuwa hawafugiki kutokana na historia zao kuwa hawajalelewa ili kufugika basi serikali ndio inafikia kuachana na watu hao kwa staili hii ya aibu.

Haiwezeni na haingii akilini serikali ya Tanzania ambayo ina Idara ya Usalama inayoheshimika duniani ifikie mahali pa kutoa kirahisi usajili kwa makundi yenye aibu na kufedhehesha Kanisa la Kikristo namna hii. Kama viongozi wakuu watasoma waraka huu basi kutakuwa na makanisa mengi ya aina hiyo ambayo hata idadi yake inaweza kuzidi hata 20 yatafungwa.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu Mwamakula pia tunapendekeza mifumo yetu ya usajili wa taasisi za dini, Makanisa na Misikiti ifumuliwe upya na serikali ipokee ushauri kutoka katika jamii ya Watanzania. Pia, tunapendekeza kuwa watu wanaohusika na michakato au vetting ya kutoa usajili katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ujimla wafanyiwe uchunguzi kuanzia kipindi cha miaka 10 nyuma ili tubaini waliwezaji pia kupitisha na kusajili makundi ya aibu kiasi hiki.

Pia, ichunguzwe kwa nini taasisi na Makanisa ambayo hayana shida yanasumbuliwa kupata usajili wakati makundi ya kihuni yanapatiwa usajili utadhani wananunua tiketi za mabasi ya Mwendokasi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 28 Julai 2024; saa 2:16 asubuhi

1722146114636.jpg
 
Utapeli utapeli..deception

Kumbe kuna maaskofu wako nyuma ya haya makanisa ya kitapeli
 
Back
Top Bottom