Kanisa la sasa ni masikini kuliko la zamani

Kanisa la sasa ni masikini kuliko la zamani

Zee Korofi

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2021
Posts
1,604
Reaction score
1,430
Hivi kwanini kanisa hili la sasa ni masikini kwa kuangalia maishaya waumini wake wengi, tofauti na la zamani? Leo hii walalahoi wengi ndiyo wenye dini, utawakuta huko Wakristo kwa wingi wao na Waislamu kwa wingi wao. Ipi shida?

Je, ni kweli ufalme wa mbinguni unatekwa na wenye nguvu, na akina Elon Musk wameshauteka? Inasikitisha unaingia kusali unaona kwa kuangalia tu kuwa hali za maisha ya waumini haziridhishi. Roho inauma sana.

Yaani kanisa la leo hasa la Afrika ni ajabu sana, halina watu wengi mashuhuri na wenye nguvu. Kanisa la Kiafrika la leo halina hata tajiri wake mmoja maarufu, wengi ni atheists na wakristo kwa majina tu. Hii aibu.

Zamani kanisa lilikuwa na watu wenye nguvu.

Manaeni - Huyu alikuwa ndugu wa kunyonya wa Mfalme Herode, kwa leo tungesema mdogo wa Rais au kaka.

Melkizedeck - Alikuwa Mfalme na Kuhani wa Mungu aliyejuu sana, alikuwa tajiri wa kutupwa. Kwa leo tungesema ni Rais badala ya Mfalme.

Timotheo - Alikuwa daktari bingwa na maarufu.

Kwa mifano hiyo michache naona mmepata mwanga kdogo wa concept yangu.

Shida ni nini? Inawezekana kumuomba Mungu Mkuu pasipo dini?
 
Dini zishakuwa biashara sio sehemu za kiroho tena

Kwa ufupi kuna ujinga mwingi sana kwa kitisho cha kifo, mateso na moto wa milele
 
Dini zishakuwa biashara sio sehemu za kiroho tena
Kwa ufupi kuna ujinga mwingi sana kwa kitisho cha kifo, mateso na moto wa milele
Mungu yupo, hivyo na hayo yapo. Imani ina nguvu.
 
Ukipata pesa hatua ya Kwanza Ni kumuacha mungu, no matter kabla ujapata ulimuomba mungu na kuahd kumtumikia, lakini Kuna tabia huletwa na pesa.
 
Dhumuni la kanisa ni utajiri? Una elewa maana ya kanisa?
Si lengo kuu la kanisa, ila ni miongoni mwa malengo ya kanisa kuhakikisha waumini wake wanaishi katika unafuu(wanawezeshana), kwani ni jamii moja tayari. Sasa kanisa la leo kwa kuona tu hivi vitu havipo, ubinafsi na utapeli umepelekea hayo.

Sijasema kanisa la leo liwe tajiri, ila nimeongea kutokana na hali iliyopo(kuwa sijaona tajiri au mtu mweusi mashuhuri duniani kwa sasa, Muafrika na anayetoka kanisa la Afrika linalotambulika)
 
Ukipata pesa hatua ya Kwanza Ni kumuacha mungu, no matter kabla ujapata ulimuomba mungu na kuahd kumtumikia, lakini Kuna tabia huletwa na pesa
Kwamba pesa ni kama msafara wa Rais wa US nchini Tanzania? Yaani inakuja na kila kitu chake wewe vitu vyako havitumiki siyo?[emoji23]

Ila siyo kwa kila mtu, kuna watu wanatawala fedha na utajiri pasipo hivyo kuwatawala wao.
 
Unakosea angalaia hao waliofanikiwa dini iliwakuta katika hali gani. Wengi walikuwa wanahangaika mfano Petro mvuvi wa samaki hata Ibrahimu n.k. wengi wlikuwa na mapepo na visanga mbalimbali Mungu akawasaidia ndio wakaanza kutumika.
 
Back
Top Bottom