Kuanzisha hifadhi za wanyama au mazingira hakuna maana kuwa taasisi binafsi au za kidini zisijihusishe na shughuli za uzalishaji mali.
Infact kama kuna jambo ambalo jumuiya ya Kikristo duniani kupitia makanisa inalifanya sasa hivi ni kujishirikisha katika uzalishaji mali ili kuinua ubora wa binadamu.
Utalii ni chimbuko la mapato, kama eneo hili ambalo kanisa inamiliki litashamiri, basi huduma za maendeleo kwa jamii kama Shule, Hospitali, maji, na mengineyo yatapatikana kwa urahisi kwa kutumia mtaji unaotokana na mapato ya uzalishaji mali na si kusubiri misaada au sadaka.
Soma Times magazine kuhusiana na Mchungaji Rick Warren anachojaribu kukifanya kuboresha maisha ya binadamu. Soma makala ya Bill Gates ya Creative Capitalism, ugundue ni vipi wenzetu wanapiga hatua na kuachana na kutegemea Serikali.
Falsa ya Kanisa kujiingiza katika huduma za jamii na hata biashara, si kujipataia fedha bali ni kutoa huduma na kushirikisha jamii.
Hii nguzo yake ni ile hotuba ya Yesu maarufu kama sermon on the mountain ambapo aliuliza nilikuwa mgonjwa, ukanitibu, nilikuwa na njaa, ukanilisha, nilikuwa uchi ukanivisha nguo, nilikuwa sina pa kulala ukanipa pango n.k.