Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Baada ya hospitali maarufu kupigwa bomu hapo jana na wagonjwa na madaktari 500 kuuliwa, leo imekuwa ni zamu ya kanisa na misikiti iliyojaa wakimbizi kuripuliwa na majeshi ya Israel.
Hayo yametokea huko Kusini ya Gaza watu walikotakiwa kukimbilia. Sambamba na kanisa na misikiti barabara vile zimebomolewa na makombora hayo ya kutoka kwenye ndege za kivita kuzifanya zisipitike kupeleka misaada inayosubiriwa kwa haraka na jamii hizo za kipalestina.
Mashambulizi yote hayo yanatokea huku umeme na maji vikiwa vimekatwa kwa takriban wiki moja sasa kwenye eneo kubwa la Gaza.
Kama kwamba lengo ni kuwaua wapalestina kwa njaa na kiu malori 20 tu yamekuwa yakipigwa danadana kuingia Gaza kwa muda mrefu kutokea kituo cha Rafah ilhali mahitaji ni tani zinazojaza mamia ya malori kutokana na kusihiwa na mahitaji yote muhimu.
Shambulio la kwenye hospitali lilitanguliwa na tangazo la takriban siku mbili likiwataka wagonjwa na madakrari kuondoka hospitalini hapo ambapo madaktari waligoma kuondoka kwa tamko la kutoweza kuondoka na kuacha wagonjwa wao.Hapo ndio likafuata bomu zito kutoka angani.
Kilichowashangaza wengi kuhusu mashambulio kwenye makanisa na misikiti ni kwamba kila aliyepata nafasi kuingia humo alihisi yuko salama zaidi kinyume na kilichowatokea.