Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mara ya kwanza hili neno nililisikia kutoka kwa prof. (kabla halijasikika mitaani wala kwenye tv) aliyekuwa anatufundisha kozi ya Lexicography; alisema Kanjanja ni mtu anayefanya kazi asiyokuwa na taaluma nayo. Alilitumia neno kanjanja alipokuwa anajaribu kufafanua jinsi kamusi zinavyoundwa....ndipo akasema..."Kuna kamusi huko mtaani zinauzwa lakini zimetengenezwa na makanjanja" akiwa na maana kwamba hao watu hawana taaluma ya uundaji kamusi (Lekskografia). Kwa hiyo nafikiri hili ni neno la kiswahili sanifu.Wadau wa lugha, ivi hili neno ni msamiati rasmi ama ni neno lililoibuka tu kuwatambulisha waandishi wazamiaji au linaweza kutumika kwa mtu yeyote?