Kwa mara ya kwanza hili neno nililisikia kutoka kwa prof. (kabla halijasikika mitaani wala kwenye tv) aliyekuwa anatufundisha kozi ya Lexicography; alisema Kanjanja ni mtu anayefanya kazi asiyokuwa na taaluma nayo. Alilitumia neno kanjanja alipokuwa anajaribu kufafanua jinsi kamusi zinavyoundwa....ndipo akasema..."Kuna kamusi huko mtaani zinauzwa lakini zimetengenezwa na makanjanja" akiwa na maana kwamba hao watu hawana taaluma ya uundaji kamusi (Lekskografia). Kwa hiyo nafikiri hili ni neno la kiswahili sanifu.