Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Huu pia sio uzi wa lugha, unaingiliana sana na siasa. Ugonjwa wa Kansa, au Kensa, au Saratani, unatajwa hivyo na wazungumzao Kiswahili kana kwamba ni ugonjwa wa kigeni kutoka nchi za mbali usiotambulika ila hivi karibuni.
La hasha. Ugonjwa wa Kansa ni ugonjwa ulikuwemo humu nchini tangu kale. Una majina mengi ya kienyeji, ila mimi napendekeza kuanzia leo tuuite jina la ' Mburasi' ambalo ni jina lake halisi kwa lugha ya Kipare.
Mburasi ni ugonjwa unaotambulika sana Upare na kuna aina ya Mburasi zinazoweza kutibiwa na wenyeji, sharti hayakuanza kupatiwa matibabu ya kisasa kama vile Kimotherapia.
Hii itafanya watu waelewe zaidi maana ya ugonjwa huu.
Kama vile hatimaye yalivyopatiwa majina ya kienyeji mambo kadhaa wa kadhaa, nataka ugonjwa huu wa Kansa uitwe Mburasi kwa vile hilo ni jina aslia la kienyeji linalowakilisha sawa sawa ugonjwa huo.
ends.