Nancyjoa13
Senior Member
- May 18, 2018
- 167
- 97
Kansa ya matiti ni miongoni mwa magonjwa yanayowatesa wanawake wengi duniani. Lakini kumekuwepo na hisia tofauti juu ya maumivu ya kawaida ambayo mwanamke anaweza kuyapata kwenye matiti yake. Baadhi yao wamekuwa wakihusianisha moja kwa moja na kansa ya matiti
-
Maumivu ya matiti yanaweza kuwa ni sababu mojawapo ya dalili ya kansa lakini sehemu kubwa ya maumivu hayo ni matokeo ya mabadiliko anayoyopata mwanamke katika ukuaji wake
-
Wataalamu wa afya ya mama wanasema uwezekano wa maumivu ya matiti kuwa kansa ya matiti ni mdogo. “Maumivu ya matiti peke yake ni kwa sehemu ndogo yanahusishwa na kansa”
-
Kuna aina mbili za maumivu ya matiti; Maumivu yanayotokana na hedhi ya kila mwezi ambayo mwanamke anapata ikiwa ni sehemu ya maumbile kibaiolojia. Aina ya pili ni maumivu ambayo husababishwa na maambukizi au kunyonyesha
-
Robo tatu ya maumivu ya matiti ni matokeo ya homoni za ‘Estrogen’ na ‘Progesterone’. “Maumivu ya matiti yanayotokana na homoni yanampata kila mwanamke”, “Haijalishi ana miaka mingapi. Kama bado anapata hedhi anaweza kupata maumivu ya matiti”
-
Mshtuko (Trauma) wowote kwenye matiti unaweza kusababisha maumivu ikiwemo upasuaji, majeraha, kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mwili na ngono zembe. Ni vizuri kumuona daktari kama maumivu ni makali sana na yanaendelea kwa muda mrefu