Kanumba hayupo filamu zipo, Diamond akifa muziki utaendelea

Kanumba hayupo filamu zipo, Diamond akifa muziki utaendelea

MimiNiMakini

Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
7
Reaction score
20
Imetoka List ya Wasanii wenye Ushawishi mkubwa Barani Africa, Diamond ametokea pia kwenye List hiyo na Mbaya Zaidi amejisifu kwamba Bila yeye bendera ya Tanzania haitapepea tena kimataifa iwapo hasa atafariki.

Inachekesha Sana, Diamond ameshajikuta kwamba bila yeye mambo hayaendi, huu ni uongo.

Kanumba alifariki watu wakaongea sana kwamba Bongo Movie haitaendelea lakini wapi, angalia hivi sasa kuna series nyingi kali, waigizaji wakali, uwekezaji mzuri sana, Teknolojia kubwa sana, Hivi sasa Vyuoni watu wanasoma Filamu, Uigizaji.

Sasa Diamond ndio anajidanganya eti akifa ndio Muziki na Wasanii wa Bongo watashindwa kufika mbali, aisee anajidanganya sana, tena usikute yeye ndio anabania hata baadhi ya wengine Kushine, Ajaribu kufa hata wiki moja then afufuke aone yanayoendelea.

Alifariki ×××× watu wakasema Nchi haitaenda lakini wapi, mbona mambo yanaenda. Kiufupi siku hizi ule msemo kwamba Pengo Halizibiki haupo kabisa, Siku hizi kuna watu wengi wanajua vitu yani ukifa tu tukikuzika ndio basi tena mwingine anachukua nafasi.
 
Kwaio ww unaona bongo movie ya Leo ni sawa na Bongo movie ya Kanumba?kuendelea itaendelea coz life got move on ila kwa mwendo wa kinyonga sana(hatutakua na maajabu). Kanumba or Diamond ni km Man u ya Furgerson au Tz ya JPM...
Mimi sio mshabiki wa Diamond bt i belive kijana deserve his respects, he moved our music to another level and kept it there...EA streaming media zote ni yy na vijana wake wapo on top (harmonize being included maana huyu nae ni yy alimtoa). Ukiwatoa hao perfomance yetu ni ya kawaida km wengine tu, hatuna maajabu just a bunch of mediocres.
 
Hivi kuna watu na akili zao wanaangalia bongo movie sasa
IMG_7484.jpg
 
Kwaio ww unaona bongo movie ya Leo ni sawa na Bongo movie ya Kanumba?kuendelea itaendelea coz life got move on ila kwa mwendo wa kinyonga sana(hatutakua na maajabu). Kanumba or Diamond ni km Man u ya Furgerson au Tz ya JPM...
Mimi sio mshabiki wa Diamond bt i belive kijana deserve his respects, he moved our music to another level and kept it there...EA streaming media zote ni yy na vijana wake wapo on top (harmonize being included maana huyu nae ni yy alimtoa). Ukiwatoa hao perfomance yetu ni km ya kawaida km wengine tu, hatuna maajabu just a bunch of mediocres.
Kwani huwezi kuchangia bila kumtaja jiwe
 
Chai jaba hajielewi kabla yake mziki ulikuwepo na baada yake muziki utaendelea. Akina mr nice walitupaisha sana sema tu walilewa sifa wakashindwa kutoboa Nigeria (huko ndipo palipomtangaza chai jaba)
 
Tuangalie upande wa pili, hivi dot.com hamuoni kuwa diamonds &others wametupotezea muziki uliokua unatutambulisha sisi kama Taifa?,kipindi hicho wimbo ukipigwa redioni au popote unajua straight huo ni kutoka TZ,but now itabidi ufikirie sana maana huwezi jua ni kutoka Harlem au Mtanzane!,SA wapige amapiano (asili yao)na sisi tupige amapiano!,kweli nchi inakwenda kasi sana,kumbuka wanamziki mahiri kabisa pale DRC waliiga upigaji wetu wa muziki, tumepotea wapi kama nchi?
 
Ukitaka asili msikilize Saida Karoli, mziki ni biashara, hakuna aliyetayari kuwekeza pesa nyingi kutafuta kusifiwa anaimba kiasili,

Aimbe kijerumani, kihispania kwangu ni sawa kwa sababu iyo ni biashara yake Ila kuimba matusi sikubaliani nae hata kidogo,
 
Tujadili ili kama kuna ujinga hapa tueleweshane ila kama kuna upumbavu tuache, moja ya vitambulisho vya utaifa no pamoja na muziki wake ,sikiliza nyimbo za sikinde, msondo,vijana, mwenge jazz etc etc utaona kabisa kuna vionjo vya muziki wa kitanzania na huu ndio ulikua utambulisho wetu,sikiliza muziki wa DRC hadi leo huwezi kujiuliza twice, utajua tu huu muziki ni kutoka DRC, sikiliza muziki wa SA kuanzia kwa akina Makeba hadi leo kwa akina do.maphorisa, aka, makhazi etc etc basic ya muziki wao ipo vilevile njoo Zimbabwe, nenda Botswana au Zambia new generation zao zinapiga muziki wao bila kuharibu asili ya utambulisho wa muziki wao, hapa kwetu ni uchafu mtupu, tembo anapiga amapiano!hii ni craze
 
Back
Top Bottom