Kanumba: Masharti manne aliyomwekea lulu ili kulinda penzi lao

Kanumba: Masharti manne aliyomwekea lulu ili kulinda penzi lao

Michael Amon

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Posts
8,768
Reaction score
3,622
529802_289719597773160_100002053662830_707128_273834368_n.jpg


BADO taifa linaombeleza kifo cha msanii nyota wa filamu za Bongo, Steven Charles Kanumba kilichotokea Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.

Kifo cha msanii huyo kinamhusisha msanii nyota wa kike wa tasnia hiyo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu' ambaye anasemekana aligombana naye kwa mambo ya mapenzi na kumsukuma.
Lulu alishikiliwa na polisi wa kituo cha Oysterbay cha jijini Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi kufuatia kifo cha mpenzi wake huyo.

Hapo ndipo kwenye habari! Kwamba, kumbe marehemu Kanumba na Lulu walikuwa wapenzi! Ni vigumu kwa watu kuamini au kukubali, lakini ukweli unabaki kuwa huo.

MWANZO WA MAPENZI
Kwa mujibu wa watu wa karibu na marehemu Kanumba ambao walifunguka baada ya kifo huku wakiomba kusitiriwa kwa majina yao, wawili hao walianza uhusiano wakiwa katika safari moja ya sanaa mjini Moshi, Kilimanjaro. Safari hiyo ilihusisha kundi zima la Bongo Movie Club.

Kanumba ndiye aliyemtongoza Lulu na kukubaliwa na kuanzia hapo uhusiano wao ulianza rasmi. Lulu alianza kwenda nyumbani kwa Kanumba bila kipingamizi.
Majirani wa Kanumba wanakiri kuwa, mara kadhaa Lulu alikuwa akifika nyumbani hapo na ilifika wakati walikuwa wakipika na kupakua kama mke na mume.

MPANGO WA KANUMBA

Kwa mujibu wa habari hizo, marehemu kumtaka Lulu kimapenzi hakukuwa kwa ajili ya kujifurahisha nafsi bali kumuoa kwa ndoa na kuwa mke na mume.

UTAMBULISHO ULISHAANZA

Kanumba alishaanza hatua ya awali ya maandalizi ya uchumba wao kwa kumpeleka Lulu kwa watu wake wa karibu na kumtambulisha.

Mtu ambaye kuna uhakika alishakutanishwa na Lulu ni msanii na mama mlezi wa wasanii Bongo, Husna Poshi Dotnata'.Inadaiwa kuwa, Kanumba alifunga safari na Lulu hadi nyumbani kwa Dotnata, Ubungo ya Riverside, Dar ambapo aliweka wazi uhusiano wake na msanii huyo na mipango ya kumuoa.

Habari za ndani zinadai kuwa Dotnata, mbali na kushtuka alimuuliza Lulu kama atatulia baada ya kuwa na Kanumba kwa lengo la kufunga ndoa ambapo msanii huyo alisema ameshatulia.
Aidha, habari zinasema kuwa, Kanumba alimhakikishia Dotnata kuhusu uhusiano wake na Lulu huku akisisitiza si wa kuchezeana.

MASHARTI 4 ALIYOMWEKEA LULU ILI KULINDA PENZI LAO

Wakiwa ndani ya mapenzi motomoto, inadaiwa Kanumba alihisi penzi lao lingeweza kuvuja kabla ya muda aliotaka yeye, hivyo alimpa masharti manne Lulu ili kulilinda penzi hilo na mikono ya mapaparazi.

SHARTI NAMBARI MOJA

Lulu hakutakiwa kuzungumza na mwandishi yeyote wa habari kuhusu uhusiano wao na kama ni kusema, basi msemaji mkuu angekuwa Kanumba mwenyewe.
"Lulu aliambiwa kuwa asije akalianika penzi lao kwa watu, hasa waandishi wa habari. Na kama ni kuliweka wazi, basi mwenyewe ndiye angekuwa msemaji mkuu"

SHARTI NAMBARI MBILI

Kanumba alimwambia Lulu anapokwenda na kutoka nyumbani kwake, alitakiwa kupanda taksi moja yenye tinted' inayopaki Kituo cha Vatican City Hotel, Sinza. Kituo hicho kipo umbali wa mita kama thelathini kutoka nyumbani kwa marehemu.

SHARTI NAMBA TATU

Lulu alitakiwa kuachana na tabia za zamani, hasa za kupatikana kwenye vilabu vya usiku huku akiwa amelewa, sambamba na kuepuka vituko mbalimbali ambavyo vingeweza kumchafua katika jamii.
"Kama vile haitoshi, Lulu alipigwa marufuku kwenda kwenye vilabu vya usiku akiwa peke yake au na kampani mbaya.

"Pia akaambiwa aepuke vituko vya hapa na pale ambavyo vikinaswa na waandishi wa habari na kuandikwa vitamharibia sifa katika jamii," kwa kutii sharti hilo ndiyo maana miezi ya hivi karibuni, Lulu alikauka kwenye vyombo vya habari.

SHARTI NAMBA NNE

Kanumba, kwa vile alishajua mipango ya baadaye na Lulu ni kuishi pamoja, alimtaka aachane na wanaume wake wa zamani na kuanza kurasa mpya na yeye, jambo ambalo Lulu alilitii.
Lakini katika yote, inaonekana marehemu alisahau kuweka masharti juu ya matumizi ya simu kwani ndiyo tatizo lililoibukia hapo na kusababisha kifo.
 
Mkubwa what is the source of this information? Otherwise it gonna be da same old story..
 
Kiukweli ya kanumba ya kwake yameisha r.l.p the great amefunga ukurasa wake,hv ww unajua utakufa kwa ki2gan??? Mapanga,ujambaz,ajali,h.I.v or mtikisiko wa ubongo?

Na lulu 2iache mahakama ihukumu ingawa haki zote n mbingun 2. Ila haka katoto mungu akasamehe bureeee coz kana nyege mshindo ndio zinazomsumbua akijitambua ataacha mpaka sasa kameshajifunza ki2 under 18 kamesha....mbele n nyuma kwishney, tuyaache hayo sasa tujenge taifa na hawa mafisadi.
 
naiamini hii habari. Juzi nimezungumza na dada mmoja askari pale Oysterbay akanisimulia the same.
 
Kiukweli ya kanumba ya kwake yameisha r.l.p the great amefunga ukurasa wake,hv ww unajua utakufa kwa ki2gan??? Mapanga,ujambaz,ajali,h.I.v or mtikisiko wa ubongo? Na lulu 2iache mahakama ihukumu ingawa haki zote n mbingun 2. Ila haka katoto mungu akasamehe bureeee coz kana nyege mshindo ndio zinazomsumbua akijitambua ataacha mpaka sasa kameshajifunza ki2 under 18 kamesha....mbele n nyuma kwishney,2yaache hayo sasa 2jenge taifa na hawa mafisadi

hapo mkuu umenena.
 
naiamini hii habari. Juzi nimezungumza na dada mmoja askari pale Oysterbay akanisimulia the same.

So kumbe haya yanayosemwa ni ya kweli. kweli nimeamini ule msemo usemao lisemwalo lipo na kama halipo bais linakuja.
 
Muda wa kumuenzi bado kaka cuz bado watu wana machungu na kifo chake hadi pale itakapojulikana hatima ya mtuhumiwa Lulu.
Hivi wewe una akili sawa sawa kweli? ni Taifa lipi ambalo linaomboleza kifo cha mbakaji na mzinzi Kanumba? na unaposema watu bado wana machungu ni wewe na nani? maana mimi usije ukanihesabu kwenye kundi la wapuuzi.

Na kama uko Interested kujuwa hatma ya Lulu yeye ni under 17 na alikuwa anabakwa na huyu mbakaji na mzinzi Kanumba. Lulu she will be Acquitted, soon or later.
 
Mbona kijijini kwao Kanumba kuna vibinti vizuri na vitamu kuliko lulu? Angechukua ka kwao asingehitaji kuweka sharti hata moja bali angejimegea bila taabu bila hofu ya kupigwa na kitu butu kichwani.............
 
Mbona kijijini kwao Kanumba kuna vibinti vizuri na vitamu kuliko lulu? Angechukua ka kwao asingehitaji kuweka sharti hata moja bali angejimegea bila taabu bila hofu ya kupigwa na kitu butu kichwani.............

na ndio maana kila siku tunasema Love is blind.
 
Hivi wewe una akili sawa sawa kweli? ni Taifa lipi ambalo linaomboleza kifo cha mbakaji na mzinzi Kanumba? na unaposema watu bado wana machungu ni wewe na nani? maana mimi usije ukanihesabu kwenye kundi la wapuuzi.

Na kama uko Interested kujuwa hatma ya Lulu yeye ni under 17 na alikuwa anabakwa na huyu mbakaji na mzinzi Kanumba. Lulu she will be Acquitted, soon or later.

I wish kungekuwa na watu japo mia kama wewe katika hii nchi ambao wanaweza kufanya mambo ya maana na kuleta mabadiliko katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom