Kanuni ipo hivi kwa mfungaji bora wa ligi kuu NBCPL msimu huu 2023/24

Kanuni ipo hivi kwa mfungaji bora wa ligi kuu NBCPL msimu huu 2023/24

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Tupo mwishoni mwa ligi kuu ya NBCPL msimu huu 2023/2024 ambapo mei 28 2024 ndiyo tamati yake
hadi sasa vita vikubwa ni Aziz Ki na Feisal katika kuibuka mfugaji bora, vita nyingine ni ya AZam fc na Simba sc kumaliza nafasi ya pili.

Sasa tukitazama katika upande wa mfungaji bora ambao wanalingana hadi sasa ni Feisal wa Azam FC na Aziz Ki wa Yanga wote wakiwa na magoli 18 lakini Aziz ki assit 7 hadi sasa huku Feisal anazo 6.

Sasa ikitoke hadi ligi inamalizika wote wamefanana magoli basi kanuni ipo hivi;

Kanuni ya 11 (Vikombe na Tuzo)
13.1. Magoli yaliyofungwa kwa njia ya kawaida yatahesabiwa kuwa na alama mbili (2), na magoli yaliyofungwa kwa njia ya penalti yatahesabiwa kuwa na alama moja (1). Mchezaji mwenye alama nyingi atatangazwa kuwa mshindi.

13.2. Katika hali ya linganisho la alama, mchezaji aliyecheza muda mchache zaidi atapewa kipaumbele.

13.3. Iwapo wachezaji watapatana katika vigezo vyote viwili hapo juu, mchezaji aliyefunga mabao mengi ugenini atatangazwa kuwa mshindi.

13.4. Katika mashindano ya mtoano, mchezaji atakayekuwa katika timu iliyofika hatua ya juu zaidi ndiye atakayetajwa mshindi wa zawadi ya ufungaji bora.
 
Mshindi halali ni yule anayeongoza kwa magoli.

Halafu huyu Fei toto ile mechi yao na Tabora alifunga magoli matatu Tabora wakiwa wananacheza na wachezaji 8.

Ukweli upo wazi mengine ni nongwa tu za Watanzania.

Ila huwezijuwa mfungaji bora anaweza kuwa Saido yule ana uwezo wa kufunga magoli 15 peke yake akawapita wote hao.
 
Salaam Wakuu,

Leo 28/05/2024 ligi kuu ya NBC inatarajiwa kufikia tamati. Licha ya mambo mengi na vita iliyopo katika mambo mbalimbali, upo ushindani mkubwa kwenye suala la mtu atakayeibuka mfungaji bora wa ligi baada ya washindani wawili (Azizi na Fei) wakiwa wamefungana kwa kuwa na magoli 18 kila mmoja.

Kumekuwa na hoja kuwa ikitokea wachezaji hawa wamemaliza kwa kufungana magoli basi mmoja wao pekee ndiye atapewa kitatu. Wapo wanaodai wataangalia aliyecheza mechi chache, wengine wanasema wataangalia mwenye magoli mengi ya penati na wengine wanadai wote watapewa kaa ilivyokuwa kwa Saidoo na Mayele msimu uliopita.

Kwa wenye ufahamu wa jambo hili uhalisia upoje?
 
Kigezo cha magoli ya penalties.
Aziz ki ana penalties Nyingi kwaiyo hapo top scorer anakuwa fei toto
 
Ikitokea wamelingana magoli...kulingana na kanuni Magoli ya penati yana alama moja ...magoli yasiyo ya penati yana alama mbili hivyo feisal atakua na alama nyịngị kumzid azizi k na atatawadhwa kua mfungaji bora
 
Kuna magoli matatu ya Fei ni fake kabisa.
Tuwe wakweli ndugu zangu
Hilo unalosema ni kweli lakini hiyo busara na sio kanuni. Wakizingatia kanuni waliyoiweka basi lazima yahesabiwa hayo ya Tabora united.
 
Back
Top Bottom