Kanuni kuu za kufuata unapoenda kuogelea

Kanuni kuu za kufuata unapoenda kuogelea

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KANUNI KUU ZA KUFUATA UNAPOENDA KUOGELEA.

Anaandika, Robert HERIEL

Kabla ya kuyachezea maji lazima utambue haya;

1. Maji hayana Mjuzi, mbabe.
2. Maji ni kiumbe hai, kwani ni chanzo cha uhai na huweza kukomesha Uhai. Unapozungumzia viumbe vyenye nguvu basi Maji na Upepo ni Moja ya viumbe hivyo
3. Usiyaamini Maji. Kwamba unayamudu.
4. Maji hunguruma wakati mwingine ili kukutisha uogope, hasa maji yatembeayo.
5. Maji huweza kutumiwa na viumbe visivyoonekana kukudhuru.
6. Maji hayapendi uchafu.

7. Maji huzamisha vilivyohai Kwa sababu hula Nafsi za viumbe, lakini huibua viumbe Mfu baada ya kuvitoa Uhai.
8. Maji husafiri sehemu Moja kwenda sehhemu nyingine Kutoka Mlimani kwenda bondeni,
Maji huhama Kwa kupwa au kujaa Kwa bahari kutokana na mvutano wa Dunia na mwezi,
Maji husafiri na kuunda mawimbi kutokana na Upepo.
9. Maji hutembea Kasi sehemu nyembamba au yenye mshuko mkali.

Ukienda kuogolea zingatia Haya.

0. Usioge au usiwe kiherehere kuwa wakwanza kuoga kwenye Maji usiyojua Kina chake. Subiri wenyeji watangulie.
Pia maji hayapimwi Kwa mguu isipokuwa Fimbo.

1. Kamwe usioge ukiwa pekeako. Hiyo ndio rule Namba moja ya Maji.

2. Usioge kwenye maji yaliyozaidi ya kitovu chako au yanayozidi mbavu zako changa. Kwa mwenye Ujuzi mdogo au Ujuzi WA kawaida.

3. Usioge bila kupewa ufafanuzi wa kijiografia wa eneo Hilo. Kama endapo kuna mkondo bahari(Ocean Current). Kwani ni hatari.

4. Usioge Mtoni nyakati au msimu wa Mvua.
Mito inatabia ya kujaa bila ya wewe kuona wakati unaogolea.

5. Kabla hujazamia ndani ya maji vuta pumzi nyingi kisha ibane huku unaiachia POLEPOLE.

6. Kama umefanya kosa Majini, ukaenda kwenye kina cha maji mengi ambayo yanakudhibiti na nyayo zako hazigusi chini, Kwa usipaniki, pili Vuta pumzi ndani nyingi kisha ibane, tatu lala horizontal kisha nyosha mikono na miguu ipanue kisha piga makasia kwenda nyuma ukielea upande uliotoka wenye maji madogo. Hakikisha unatoa pumzi kidogokidogo.

7. Kama utaanza kukosa pumzi, vuta kidogokidogo maji Kwa njia ya pua uyatolee mdomoni. Hii iwe last step. Usivute maji Kwa mdomo utapaliwa.

8. Kama hujui kuogelea, usiende kuogelea mbali Kwa kumtegemea Mtu kuwa atakuokoa. Dakika moja inatosha maji kukuua.

9. Usioge Maji ya baridi Sana. Yanaweza fanya mapafu Kufeli kufanya kazi. Na kukupelekea kufa.

Usipende mchezo na Maji.
Maji hayachezewi.
Hasahasa Maji yasiyo tembea Kama Bahari ndio usipendelee kuleta sifa.

Expert wote wa Maji wanajua kuwa Maji ni hatari na hawanaga mchezo nayo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Maji ni kiumbe? Na yenyewe yanazaa na kuzaliwa?
Na yenyewe yanakua?
Na yenyewe yanakula?
Na yenyewe yanapumua?
Na yenyewe yanasense?
Na yenyewe yana DNA/RNA?
Na yenyewe yanajamiiana?
Na yenyewe yana regulate mazingira (homeostasis?)
 
Back
Top Bottom