Uchaguzi 2020 Kanuni mpya CCM: Tumaini la pekee la Makonda, Mtulia, Mtolea, Nassari, Mwakyembe na Mwanri ni Kamati Kuu ya CCM chini ya Rais Magufuli

Atakavyoamka siku hiyo hajasema kuwa atahamisha mtu kutoka kusini akagombee kaskazini. Na kanuni za chama zipo wazi kuwa majina matatu ndio yataenda kamati kuu kujadiliwa, washindi watatu wa mwanzo.
Sio kanuni ni atakavyoamka
 
Watu mnakuwa wa ajabu,Magu angetaka apite angepita Kigamboni,huko kapigwa chini na kamati itampiga chini
Watu hawawi wa ajabu bali wasiwasi wao unatokana na tabia ya Chama Tawala kubadili gia angani wakati wowote. Kamati ina wajumbe wachache sana inakuwa rahisi zaidi kugawa bahasha nzito hata kubadili misimamo ya Chama kama ipo. Kikao cha Kamati kinaongozwa na Mwenyekiti ambaye maamuzi yake yanategemea alivyoamka siku hiyo ielewke kuwa wahusika waliotupwa na kura za maoni ni wapendwa wake. Mwenyewe kwa kauli yake amesema na amewahi kufanya kuwa wa kwanza anaweza kuwa wa mwisho na wa mwisho akawa wa kwanza ndo maana orodha yote ya wahusika wa kura za maoni inawakilishwa kwenye Kikao cha uteuzi cha Kamati. Waliotemwa na kura za maoni walikuwa na kazi za madaraka makubwa lakini kwa maagizo toka juu waliyaacha kwenda kugombea Ubunge na nafasi zao kujazwa mara mojà kukiwa na uhakika wa kupita kwenye kura za maoni lakini hata hivyo hakuna lililoharibika Mpendwa atarekabisha. CCM mpya na mapya!
 
Kosa jingine la kiufundi litakalo izamisha ccm kwenye uchaguzi mkuu, haiwezekani kamati kuu ya watu 24 tu kuwa na maamuzi ya kibabe.
 
R

Rushwa ipo aisee! Tena rushwa kubwa mno. Fanya restrospective investigation utapata ukweli.
 

Iweje tuandikie mate na wino upo? July 27 sio mbali. Ukweli utataradadi.
 
Hilo ndiyo la msingi kuwa tumemuonyesha mteuzi wao kuwa hao watu hatuwahitaji.

Uchaguzi wa ndani wa wagombea ndiyo ilikuwa njia ya kutolea sauti za watawaliwa kwa mteuzi kuwa watu wake anao wateua kutuongoza hatuwataki.
Haya hayatuhusu muhimu ni hakubaliki...full stop!
hata akimbeba ampe unaibu waziri mkuu atajua mwenyewe
 
Swadakta
Aiseee. Muhimu zaidi wanaoitwa wanyonge huku chini wamesha amua. Hayo ya kamati kuuu hayata badili mtazamo mpana wa jamii husika juu ya hao walio kataliwa.

Wakipitishwa na kamati kuu ni sahihi na haki wakiitwa wagombea wa viti maalumu.
 
Siyo rahisi kurudishwa mtu ambaye amepata kura 2 akaondolewa aliyepata kura 200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…