Wasalaam,
Upo mchakato wa kuongeza na ama kuingiza sekta binafsi katika ununuzi wa kahawa mbivu kutoka kwa mkulima(Cherry) . Hii itasaidia kupitisha kahawa nyingi zaidi katika mitambo ya kati (CPUs) na hivyo kuongeza ubora wa kahawa husika.Hatua hii kwa upande mwingine italeta matumaini madogo kwa mkulima na baadae zao hili litakufa.Kwa machoni unaonekana ni mkakati wa kuboresha lakini ukiangalia kwa mapana yake ni mkakati chimbia kaburi kwa zao hili.Mkakati huu utaleta uvunjaji moyo wa hali ya juu kwa mkulima.
Msimu huu wa 2010-11 waninizi binafsi wamenunua hadi shilingi 600 kwa kilo ya kahawa mbivu ( sawa na Sh 3000) kwa kahawa kavu (parchment) .Na akishanunua hivyo ameondoka haangalii kwamba kuna malipo ya pili baada ya uuzaji wa kahawa hiyo ndani na/au nje .Haangalii kwamba kuna agro inputs zinaitajika kwa mkulima ili zao liwe endelevu.
Vyama vya wakulima wamekuwa wakinunua Sh 2,500 ya kahawa kavu wakihakikisha wanampatia mkulima agro - inputs za thamani ya sh 250 na kumrudia mkulima baada ya mauzo ya kahawa hiyo ( soko la nje au ndani ) kwa malipo ya pili (final payments) .Sasa kwa sababu wakulima wanataka pesa ya saa hiyo hiyo watakimbilia kuchukua Sh 3000 za private buyers baadae watashindwa kumudu agro inputs ( mbolea na madawa ) na ndio utakuwa mwisho wa zao hilo.