Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanzisha kanuni mpya kwa ajili ya shughuli za kubadilisha fedha za kigeni, ikijumuisha uwepo wa masharti makali zaidi kwa ajili ya miamala inayozidi dola za Marekani 5,000. Kanuni hizi mpya zina lengo la kuimarisha uwazi, uwajibikaji, na usalama ndani ya soko la fedha za kigeni.
Matokeo chanya:
Kanuni hizi mpya zina matarajio makubwa ya kuleta athari chanya haswa kwenye soko la fedha za kigeni nchini. Baadhi ya faida zinazotarajiwa kuonekana ni uwepo wa kanuni hizi zitasaidia kuimarisha uthabiti wa uchumi kwa kudhibiti mtiririko wa fedha za kigeni na kupunguza hatari ya uhalifu wa fedha pamoja na utakatishaji fedha.
Pia kwa kuweka masharti makali zaidi kwa ile miamala mikubwa, kanuni hizi zitasaidia kuongeza uaminifu katika soko la fedha za kigeni pamoja na maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, na hivyo kuvutia wawekezaji wa kigeni.
Mbali na hivyo masharti haya yatakwenda kuimarisha udhibiti wa miamala, kwa sababu kanuni hizi zitasaidia kupunguza uhalifu wa fedha kama vile ugaidi na biashara ya dawa za kulevya. Kubwa zaidi ni kuwa kanuni hizi zitasaidia kuongeza ufanisi wa soko la fedha za kigeni kwa kuweka viwango vya ubora na uwazi.
Matokeo hasi:
Hata hivyo, pamoja na faida zinazotarajiwa, kanuni hizi mpya zinaweza pia kuleta athari hasi kwenye soko la fedha za kigeni. Baadhi ya athari hizi ni kuongeza gharama za biashara, kwani kanuni hizi zinaweza kuongeza gharama za biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao wanategemea sana kubadilisha fedha za kigeni, hivo gharama za bidhaa ama huduma pamoja na uendeshaji zinaweza kupaa maradufu.
Upande wa pili ni kuwa kanuni hizi zinaweza kupunguza ufikivu wa huduma za kubadilisha fedha katika maeneo ya vijijini na mbali, ambapo kuna idadi ndogo ya mabenki na taasisi za fedha, maeneo yasiyo na huduma za kifedha ni ngumu kupata maduka haya ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kuwa gharama za uendeshaji zitakuwa ni kubwa ukilinganisha na wakati ambao kanuni hizi hazikuwepo kwenye mfumo.
Ni suala ambalo kila mtu anaweza kukubaliana na mimi, kanuni hizi zinaweza kuongeza muda wa kusimamia miamala, na hivyo kuchelewesha biashara na shughuli za kibiashara.
Uwepo wa IFU kwenye mifumo ya kifedha hutoa msaada mkubwa katika kufuatilia kwa ukaribu shughuli haramu kama utakatishaji wa fedha, hivyo tunaweza kukutana na suala la kuongezeka kwa muda wa kusimamia miala hii.
Ni dhahiri kuwa kanuni hizi zinaweza kusababisha kuongezeka kwa uhalifu wa fedha katika soko la haramu la fedha, ambapo watu wanaweza kutafuta njia za kubadilisha fedha nje ya mfumo rasmi, hapa ndipo vishoka huingia kazini na katika hili ndipo fedha feki huingia kwenye mifumo na jamii hujikuta wakizitumia katika shughuli zao.
Kanuni hizi mpya za Benki Kuu ya Tanzania mahususi kwa ajili ya shughuli za kubadilisha fedha za kigeni zinaweza kuleta matokeo chanya kwenye soko la fedha za kigeni.
Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kuwa matokeo hasi yanayoweza kutokea katika kipindi hiki, na kuchukua hatua za kupunguza madhara hayo kwa kushirikiana na Wizara ya fedha, Hazina, pamoja na vyombo vya usalama kama vile Uhamiaji, Jeshi la Polisi pamoja na Usalama wa Taifa katika kupunguza athari za matokeo hasi.
Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa kanuni hizi zinatekelezwa kwa ufanisi na uwazi, ili kuepuka kuongeza mzigo usio wa lazima kwa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida.
Kwa kufanya hivyo, Tanzania inaweza kuendelea kuimarisha uthabiti wa uchumi wake na kuvutia wawekezaji wa kigeni. Pongezi nyingi sana Emmanuel Mpawe Tutuba, pamoja na timu yako haswa Dr. Yamungu Kayandabila.