Kanuni muhimu kwenye kuutafuta uhuru wa kifedha

Kanuni muhimu kwenye kuutafuta uhuru wa kifedha

josephdeo

Member
Joined
Nov 23, 2015
Posts
95
Reaction score
207
Kitabu changu cha mwisho kusoma mwaka 2021 ni THE RICHEST MAN IN BABYLON.

Ukizungumzia kati ya dola kubwa za kale babeli ni moja wapo kati ya hizo ambazo zitakuwa kwenye list. Hivyo muandishi alitaka tuelewe ni kanuni zipi ambazo zinaweza kukusaidia wewe kuufikia uhuru wa kifedha. Hapa tutaweka fact hizo kwa lugha ya kishikaji ili kuwa rafiki kwako kijana wa kisasa

Sura ya kwanza anaelezea marafiki wawili ambao walikuwa ni mpiga kinubi na fundi wa magari ya farasi ambao walionana na kuanza kujadili kuhusu hali zao yaani umasikini uliotukuka. Kilichofanya mpaka wajadili hayo ni baada ya mmoja kuota ndoto akiwa na dhahabu nyingi sana.

Kwenye ndoto alikuwa tajiri lakini kwenye maisha halisi alikuwa fara fulani hivi sema mtaalam sana wa maswala ya ufundi. Katika majadiliano hayo mmoja wao anatoa taarifa kuwa kuna mwana ambae walipiga nae skuli na wakawa pamoja enzi za ujana wao lakini yeye aliwapiga gepu kubwa kwani alikuwa tajiri ambaye hata angetumia vipi mali zake asingefirisika.

Wote kwa pamoja wanafikiana kuwa wamtafute mwana ili awape madini kwanini kafanikiwa alafu wao bado wako kwenye tagi ni ubavu wao (mtaji wa masikini ni nguvu zake). Wanapanga siku wanakusanya na wana wao wengine wanatimba kwa mwana kupata somo. Mwana yule tajiri hakuwa na hiyana si unafahamu kuwa yeye nywele zake sio ngumu kama zetu.

Hivyo kuwapa hashtag wenzake watoboe sio inshu kabisa. Hivyo anaanza kutoa madini kwa kuwaambia kuwa walishawahi kujifanyia malipo wao?. Wote wanashangaa wengine wanaenda mbali zaidi kwa kumwambia mwana kuwa wao hawakufuata stori za Abunuasi na ndoto za mchana bali madini ya kupata utajiri.

Mwana nae akawakazia kwa kuwaambia kuwa huo ndio utajiri wenyewe. Pia anaamua kuwafafanulia ni namna gani kujilipa mwenyewe kunavyokuwa na kunaendana vipi na utajiri. Si ngozi nyeusi tu ambao ni wagumu kuelewa kwani hata hizo ngozi nyeupe nao ni bateo (huu ni msemo wa kisukuma kumaanisha hamna).

Mwana anawaambia kuwa na yeye wayback alikuwa anapiga michongo kwenye maktaba. Kitambo hiyo hakuna printer hivyo shughuli zote za kuchapa zilifanyika kwa mikono na mwana ndio ilikuwa michongo yake. Siku moja akiwa kwenye harakati za kusababisha njia ya chooni isiote nyasi akaja tajiri mmoja ambae alikuwa na shida ya kunakiliwa sheria ya tisa (hii sijui ilikuwa na maana gani ila elewa hivyo hivyo kwa sababu sio ya maana sana).

Mwana akapewa siku tatu kukamilisha huo mchongo. Siku tatu zikasanda mchongo haujamalizika (sipati picha angekuwa kwenye utawala wa awamu ya tano). Tajiri yule akarudi na kufoka mno kama underground anapopewa shavu la kusikilizwa na producer Majani. Jamaa akamuomba tajiri yule kuwa ataifanya kazi hiyo kwa usiku mzima ili tu tajiri yule ampe siri ya mafanikio. Deal ikawa done

Mwamba akajipinda usiku mzima kwani hata yeye aliuchukia umasikini kama ilivyo kwa mimi, wewe na yule. Akafanikiwa kumaliza na alipomaliza mzee akaja na kumwambia kuwa anatakiwa kujilipa asilimia kumi ya pato lake. Mwana hakuelewa mzee ikabidi kumuelewesha kuwa kama ambavyo anapay bill zake basi na yeye ajiweke kwenye hizo bill na kujilipa kwa asilimia hizo kumi.

Kisha baada ya kutunza hicho kiwango hatua inayofuata ni hahakikishe kuwa pesa hiyo anaiweka kwenye uwekezaji. Yaani kama umepata tembo (elfu kumi). Kwenye kutunza pato lako kwa asilimia kumi basi hakikisha hiyo pesa unaiwekeza kwenye chochote ambacho kitaidhalisha.

Wakati mwingine wanachotuzidi ngozi nyeupe ni usimamazi tu kwani sisi weusi ni kama tunakauzembe kwenye hilo. Mwana akaanza kufuatisha hiyo kanuni hiyo ambapo alitunza kwa mwaka mmoja asilimia kumi ya pato lake. Baada ya kupata akampa mtengeneza tofali ili akamununulie vito.

Mwana alipigwa hiyo pesa huku mzee yule akimpa shutma kwa kumwambia kuwa ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Hivyo hakupaswa kumpa mtengeneza matofali kazi ya kununua vito. Bali kazi hiyo alipaswa kumpa sonara.

Kupotea njia ndio kuijua waswahili hawakuwa wajinga kusema hivyo. Kupigwa kwa bwana yule kukawa funzo kwake kuwa kimfaacho mtu chake. Hivyo akatunza tena na kuwekeza tena na hiyo ikawa siri ya mafanikio yake. Kwani aliwezesha asilimia kumi zile kuziwekeza na kuzizalisha kisha uzalishaji huo ukamfanya kuwa THE RICHEST MAN IN BABYLON. Just to make a long story short.
 
Niliskitika sana nilipojua hao ni wahusika wa kubuni tu,ni kitabu kinachovutia
 
Mkuu jambo nililoambulia hapa ni kwamba katika vipato vyetu,akiba haitakiwi kubaki tu bali inabidi na yenyewe iingizwe kuzalisha,sijui ndio hivyo au la
 
Back
Top Bottom