ONJO
JF-Expert Member
- Jun 1, 2022
- 216
- 265
Habari zenu wakuu,
itifaki imezingatiwa
Ndugu zangu jua lilikuwepo tangu zamani na mpaka sasa hivi tunaona uwepo wake.
Mwezi ulikuwepo tokea zamani mpaka sasa tunauona mwanga wake.
Mvua ilikuwepo tokea zamani nayo inanyesha nyakati zetu.
Tokea zamani mvua,mwezi na jua vilifanya kazi yake bila kuchoka kwa watu wote.Mpaka wakati huu vinafanya kazi ile ile ya zamani nyakati zetu.
SWALI. Je,kama jua halichoki kutoa mwanga wake mchana na sisi Binadamu tumetoa nini kwa jua?
Je kama mwezi hauchoki kutoa mwanga wake usiku,sisi Binadamu tumetoa nini kwa mwezi?
Je kama mvua haichoki kunyesha kila mwaka na sisi Binadamu tumetoa nini kwa mvua?
Hiyo ndiyo asili ya dunia tukaayo ndani yake,hutoa bila kutegemea chochote.Asili hiyo hututaka kila mwanadamu kutoa au kusaidia bila kutegemea chochote.Binadamu yeyote akitenda tofauti na hiyo asili yenyewe humkataa kupitia ndugu na jamii inayomzunguka.
Kanuni ya kutoa ni kuwa nacho.Kikiwa kikubwa unatoa sehemu yake,na kikiwa kidogo unatoa sehemu yake pia.
KUTOA KWENYE MAHUSIANO YETU
Wengi wetu tumeumizwa kwani tulitoa tukitegemea kitu flani badae tutapata.Mfano unampa binti mrembo elfu 40,ukiwa na lengo la kumla baadae pengine unakuta huyo binti hata hana hisia na wewe kimapenzi.Badae anakukataa;hapo ndipo lawama inapoanzia.Basi tujueni kwamba tukitoa au kusaidia mtu kwa kutegemea kitu flani tujue wazi kwamba hakika tataumia,na kwa namna nyingine hii tnaita ni biashara.Na biashara kazi yake kuu ni kutafta faida.
Tukubali tukatae ukweli ni kwamba mtu anayetoa kitu au kusaidia,mfano pesa bila kutegemea chochote hujikusanyia marafiki wengi wa jinsia zote.Na hapa huwa ni fursa kwake kwani watu wote watampenda na kujiweka wazi kwake kwa kila fursa iyoonekana.Na ni sehemu nzuri kwa mdada au mkaka kujua tabia za watu na ni rahisi kwake kujipatia marafiki wenye moyo safi pamoja,wachumba,pamoja na wake.
NB.Tabia nzuri ya watu ipo katika kutoa.Mfano kusaidia wenye uhitaji,kujitolea kufanya kazi na kadhalika.Na kutoa hakuna mwisho hata kama unampa mtu yeye yule kila siku.
Tuukubali ukweli maana ndiyo asili ya dunia yetu.Kwa wanaume/mwanamke ukimpata mdada/mkaka ambaye ameteka moyo wako.Inafaa ujitoe kwa hali na mali kwa sababu ndiyo asili ya dunia.
NB:mfano Ukiona mwanaume kaombwa hela na mwanamke na akakataa au akarudisha dharau jueni wazi kwamba huyo hana moyo wa kutoa na anapingana na ukweli wa dunia.
Na mwanamke naye akifanya hivyo kulingana na mahitaji yaliyopo anapingana na kweli.
Inawezekana kupitia kutoa tkadharaulika lakini msimamo wetu uwe wa kutoa daima maana kupitia kutoa tunapanda tusichokijua chenye manufaa kwetu.
Basi kutoa au kusaidia watu ndiyo iwe furaha yetu siku zote.
Na ONJO Mpenzi wenu.