Kanuni ya mtetemo/peponi vs kuzimu

Kanuni ya mtetemo/peponi vs kuzimu

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
KANUNI YA MTETEMO/PEPONI VS
KUZIMU

Imeandaliwa na kuandikwa na Dogoli kinyamkela

1736185903846.jpg


🗣️Hakuna kinachopumzika, Kila kitu kinajongea, Na kila kitu Kiko kwenye mtetemo/kinatetema.

✍️Kila kitu kwenye huu ulimwengu kina jongea, Iwe wanyama, sisi na hata zile object ambazo Zina masafa ya mitetemo(Vibrational frequencies).

🤏Hii kanuni inasema kwamba tunaweza kuvivutia (attract) vitu na nishati kwa kutumia haya masafa yetu ya mitetemo (vibration).

🤔Hii mitetemo ndiyo inayoshawishi haya matukio unayoyaona kwenye maisha yetu na hata kwenye huu ulimwengu unaotuzunguka.

🧖Hata mawazo yetu Yana baadhi ya mitetemo, Na hii mitetemo hubadilika kutokana na hisia zetu tunazokuwa nazo katika muda husika.

✍️Kama ukiweza kuitumia hii kanuni Basi hakika utaweza kuukontroo uwezo wako wa kiakili.

🚶Watu ambao wako katika mitetemo ya chini wao ndiyo ambao muda wote Wana mawazo mabaya, hisia Kama za aibu, Uoga, wasiwasi, Hasira, Hatua nk.

🧘Lakini watu ambao wako kwenye mitetemo ya juu, wao mawazo yao na hisia zako ziko katika vitu vizuri, Mfano Kama upendo, amani, Kukubalika na kutaalamika.

👯Na pale inapotokea unakutana na mtu ambaye mitetemo yake iko tofauti na wewe Basi masafa au frequencies za hii mitetemo huongezeka,na ndiyo maana inashauriwa kwamba Ni vizuri kuwa karibu na watu ambao mitetemo yenu inafanana.

🗣️Jaribu kuangalia katika ushabiki wa mpira, pale mnapokutana watu mnaoshabikia timu mbili tofauti, Kisha mkaanza kubishana kila mmoja akivutia kwake, hapa automatic tu haya masafa yataanza kuongezeka na kila mtu atajikuta anaitetea timu yake kwa nguvu Sana tofauti na Mara yakwanza na Kama msipokuwa makini Basi mnaweza kupigana na kusababisha maafa makubwa Sana.

✍️Na hii pia IPO hata katika mabishano ya Imani pale ambapo kila mtu anaposhabikia Imani yake, Basi hapo mtajikuta mnatumia nguvu kubwa Sana na mwisho wa siku kupelekea Ugomvi au maafa kabisa, Ni hii hii mitetemo ambayo huongezeka na kupungua Kulingana na tukio husika.

🔥Hii mitetemo ndiyo ikaja kuleta kauli kwamba Kuna watu wanaishi motoni/kuzimu na Kuna watu wanaishi peponi Ikiwa bado wapo hapa hapa duniani.

🧖Hapa Sasa unakuja kuona kwamba kumbe peponi na kuzimu siyo sehemu Kama ambayo tumekuwa tukiwaza, Ila Ni uwanda wa hii mitetemo katika ulimwengu wà akili.

🤷kuzimu Ni sehemu ya masafa ya chini Sana ya hii mitetemo na huku ndiyo kwenye Mambo mengi ya aibu, majanga, kusengenyana, kuchukiana, yaani huku hakuna zuri ambalo utafanya na linaonekana Kama zuri huku kuzimu watu wa huku hawatakumbuka mema uliyoyafanya wao kila kitu kwao Ni kibaya tu, hii Ni kutoka na hayo masafa ya mitetemo ya chini ambayo ndiyo yenyewe yanamiliki hizo hisia za majungu.

🗣️Lakini peponi Ni uwanda wa juu Sana wa hii mitetemo ambako huko Kulingana na mitetemo yake, Basi huko upendo umetawala, amani imetawala, furaha na Mambo mazuri yote yanapatikana huko, huko Ni uwanda ambao Kuna hisia chanya tu na Wala siyo hisia hasi, huko hata mtu akikusema haukasiriki maana unaona kabisa hajanisema kwa kunionea Ila Ni moja ya SoMo amenipa.

💃Huko hata mtu akiumwa halalamiki Ila anaelewa kwamba mwili magonjwa Ni sehemu yake Ila Mimi Sina magonjwa.

👌Lakini haya yote yanafanyika katika Uwanda wa akili na hisia tu na mwisho wa siku hujileta kwenye udhihilisho wa mwili yakiwa Kama matukio au tabia husika ya mtu.

👀Hii mitetemo ndiyo wakati mwingine inafanya hata mtoto mdogo aweze kucheza na nyoka kwa sababu hakuna mitetemo ya hofu pale, lakini wewe mzazi ukija na mitetemo yako ya chini unaanza kupiga kelele utafikili mtoto kagongwa kumbe walikuwa wanacheza tu na Yule nyoka.
 
Back
Top Bottom