JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kanuni ya Ushirika ni kanuni iliyowekwa katika Ibara ya 7(1) (d) ya mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Treaty, 2007) inayotaka maamuzi yoyote ya Jumuiya yaanzie ngazi ya chini kabisa ambayo ni wananchi.
Kanuni hii inatoa nafasi kwa wananchi kujadili na kuamua mambo yote ya Jumuiya kabla ya wakuu wa nchi kuamua kulingana na wananchi walivyoamua katika nchi zao juu ya jambo husika.
Kushindwa kuwapa nafasi wananchi ya kufanya maamuzi juu ya jambo lihusulo Jumuiya, maamuzi yatakayotolewa na wakuu wao yatakua yamekiuka kanuni hii na yatakuwa batili.
Upvote
2