Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Kuwaona wengine walivyo kupitia wewe "Prophetic Codes"
Tunashindwa kufikia hatma na kuishi katika asili yetu kutokana na kupuuzia au kuyaona mambo katika muono wa kawaida, kupuuzia na kutojifunza kabisa juu ya tunayo yaona.
Wachache waliofanikiwa kuweka umakini kwenye masuala yanayochukuliwa kama mzoea na wengi wetu leo tunawaona kama watu wenye bahati na uwezo wa kipekee Duniani.
Kuna baadhi ya mambo tukiyatilia umakini tutaufahamu uwezo ambao Mungu ameweka ndani yetu. Waliofanikiwa kuweka umakini katika baadhi ya mambo hayo leo wanautazama ulimwengu katika namna ya kiumbaji.
Yaani wanaweza kuleta msawazo wa nguvu zao kuumba wayatakayo. Uwezo huu kila mtu amejaliwa na Mungu lakini tatizo ni kupuuzia kwetu. Baadhi ya kanuni za kuweza kuingia katika maisha ya mtu mwingine na kuona ni:
1. Kuwaza (mawazo). Tabia au hali ya kuwaza inaweza kumuwezesha mtu kufanya vitu au kwenda sehemu tofauti tofauti. Ikumbukwe mwanadamu ana uwezo wa kuwa mawazo yake yalipo.Tuna weza kufanya vitu vingi sana katika mawazo yetu hata dhambi huanzia katika mawazo.
Jizoeshe kutokuyapuuzia mawazo yako kwani yana maana fulani kwako. Unachokihitaji kutoka hapo ulipo siyo zaidi ya mawazo yako. Yusufu alipoazimia (alipowaza) kumuacha mchumba wake Mariamu tunaona Malaika akimtokea katika ndoto na kumpa faraja.
Kabla ya Kaini kumuua nduguye (Habili) tunaona Kaini aliwaza kufanya hivyo na Mungu kutokana na rehema zake alimtahadharisha Kaini juu ya wazo lake ila Kaini hakuweka umakini kama ilivyo kwetu leo. Mungu hana upendeleo anazungumza na kila mtu, mwema na mbaya.
Angalia kipindi Abrahamu anaingia Misri Farao alimtamani Sara( Mkewe Abrahamu) lakini Mungu alizungumza na Farao kumtahadharisha licha ya matendo maovu ya Farao.
Mungu anaweza kuzungumza na wewe wakati wowote bila kujali hali yako tatizo ni utayari wako kusikia kwa sababu hakuna mtu ambaye Mungu hazungumzi naye. Unaweza ukastuka ila hata Shetani huwa anazungumza na Mungu.
2. Subira na usikivu, Ili uweze kupata jibu la unachohitaji inakupasa kuwa na uwezo wa kusubiri na kusikia. Unapowaza juu ya kitu au mtu maana yake umejihusisha naye au umejihusisha na hicho kitu na Ili uone matokeo sharti subira na usikivu viwepo.
Wazo ni mbegu sharti pawepo na muda wa kusubiri na kuangalia mpaka mbegu kuota. Kuwaona wengine kupitia wewe kinaweza kuwa katika namna ya mawazo. Jiulize unapomuwaza mwingine unasikia nini. Hii ni moja ya siri wanayotumia manabii wengi wanapotaka kuelewa na kueleza maisha ya mtu mwingine. Kumbuka unapoyafanya hata yote sharti uwe na imani.
...........itaendelea............