Michael nguma
New Member
- Jul 26, 2022
- 4
- 2
Mwenye macho namwambia atazame na asome ijapokuwa imesemwa mwenye macho haambiwi tazama.
Hizi mbio sio zetu, wametulazimisha, tumekimbia kuliko uwezo wetu, tumeanguka, hatuwezi kuinuka tena, saivi wao ndio wanatuinua, saivi wao ndio wanatetembeza. Hatuna pumzi tena mapafuni mwetu.
Sera za maendeleo kati ya mataifa tajiri na mataifa maskini haziwezi kufanana. Inashangaza leo duniani, kuona mataifa maskini yakijiwekea sera za maendeleo zinazofanana na sera za maendeleo za mataifa tajiri. Mataifa maskini yamejiingiza kwenye mbio zisizo zao, mbio za mataifa tajiri zina kanuni za kitajiri ambazo mataifa maskini hayawezi kuzimudu.
Mataifa maskini yamejikuta katika hali ya kutokujiweza kwa sababu za kutumia kanuni za maendeleo zinazofanana na zile za mataifa tajiri, mataifa maskini yamekuwa mzigo kwa mataifa tajiri, mataifa tajiri yanayakokota mataifa maskini, mataifa maskini yameshindwa kujiinua yenyewe, mataifa maskini yanainuliwa na mataifa tajiri, mataifa maskini yameshindwa kusimama yenyewe, mataifa tajiri yanayasimamisha mataifa maskini, mataifa maskini yameshindwa kutembea yenyewe, mataifa maskini yanakokotwa na mataifa tajiri. Mataifa tajiri yanacheleweshwa na mataifa maskini.
Ndipo sasa mataifa tajiri yanapopata nguvu za kuyafanya mataifa maskini chochote yanachotaka. Ndipo sasa mataifa maskini yanapoanza kutawaliwa na mataifa tajiri, maana mataifa hayo maskini hayawezi kusimama mpaka yasimamishwe na mataifa tajiri, hayawezi kutembea mpaka yakokotwe na mataifa tajiri wala kuinuka hayawezi mpaka yainuliwe na mataifa tajiri.
Ni heri mataifa maskini yakayaacha mataifa tajiri yaende, ni heri mataifa tajiri yakakubali kuyaachia mataifa maskini yatumie mwendo wao.
Kanuni za maendeleo zinazofanana kati ya tajiri na maskini zinaua kabisa maendeleo kidogo aliyo nayo maskini, zinamfanya maskini awe tegemezi kwa tajiri, zinampa tajiri nguvu za kumtawala maskini
Huwezi kuandaa mbio kati ya mtu mzima na mtoto mchanga. Kama utaandaa mbio kati ya mtu mzima na mtoto mchanga, uwe na uhakika kuwa huyo mtoto mchanga atakufa au atazimia au atamchelewesha huyo mtu mzima. Hiki ndicho kinachotokea kati ya mataifa tajiri na mataifa maskini na kati ya tajiri na maskini.
Ni nani asiyejua kuwa mataifa maskini yamekuwa mzigo kwa mataifa tajiri? Ni nani asiejua kuwa mataifa maskini yanayachelewesha mataifa tajiri? Ni nani asiejua kuwa mataifa maskini hayawezi kusimama yenyewe pasipo mikopo na misaada kutoka kwa mataifa tajiri? Ni nani asiejua kuwa mataifa maskini hayawezi kujiendesha yenyewe kibajeti pasipo kuendeshwa kibajeti na mataifa tajiri?
😭😭😭 NI NANI MMOJA WENU ASIEJUA? 😡HII NI KWA SABABU YA KUFANANA KWA KANUNI ZA MAENDELEO KATI YA MATAIFA TAJIRI NA MATAIFA MASKINI.

Upvote
0