Kanuni za mpira tulipokuwa watoto

Kwa shule ya msingi ukijua kuupiga mwingi visichana vingi vinajipendekeza Kwako Aisee Kama sasahivi Kwenye professional game.

Ukiumia unavumilia hauchechemei ili nyumbani usijulikane kuepuka kugombezwa au kuchapwa viboko au kukandwa kwa nguvu na maji ya moto sehemu iliyoumia au kunyimwa ruhusa siku kadhaa za kucheza ( banned)

Mchezaji wa timu moja akifanyiwa rafu mbaya hakuna free kick Bali timu ya upande wa pili inalipiza kwa rafu nyingine na hapo mechi nzima inakuwa piga nikupige ya rafu na Mchezaji mmoja baada ya mungine anatoka Mpaka wote wanaisha ni Mpira unakuwa umeisha.

Na kuna mechi za vitenesi ( mpira wa tennis) Wawili against Wawili au mmoja against Mmoja , upande utakaoanza kufungwa 3 Kama ni 3-2 au 3-1 au 3-0 unatoka inangia timu nyingine
 
Kwa haya ulioandika kweli ulicheza mpira utotoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpira wa utotoni nimecheza sana.

Nakumbuka nilipokuwa darasa la pili na la kwanza, jirani yetu kulikuwa na mji una uwanja unatosha kuchezea mpira.

Basi vijana wa mitaa hiyo under 17 tulikuwa tunakusanyika.

Tukiwa wengi tunajigawa timu tatu au nne, timu ikifungwa goli inatoka inaingia nyingine.

Mnacheza hadi kigiza kinaingia,. Mnaanza kutawanyika.

Unarudi home kwa kujificha, sometime hata uogi unalala

Ila siku hizi ukipita mitaani hata madogo hawachezi kama enzi hizo.
 
Giza likiingia mnamaliza mechi kwa kauli mbivu ya "kwa leooo kwa leooo" baada hapo magoli yanang'olewa na kwenda kuhifadhiwa sehemu salama.
 
Sahihi Sana[emoji2][emoji2][emoji2] hii inanikumbusha mbali sana
 
Mpira wa utotoni miaka ya 80s na 90s na 2000s mwanzoni mambo yalikuwa supa.

Sijui nani alikuwa analeta mbinu(tactics) za kuujua na kuelewa vuzuri mpira wa miguu ili mchezaji kuwa bora zaidi.

Nimekumbuka hii michezo;

1. SAFA(suffer) BWEGE
Hapa wachezaji mnakuwa kwenye mpagilio wa mzunguko(round) kisha mchezaji mmoja (BWEGE) anaingia kati na kutafuta mpira mpaka aupate.

Anayeupoteza kwa BWEGE ndiye ataingia kati na kuchezeshwa kama BWEGE. Maana wachezaji wengine wanapasiana mpira wakiwa kwenye ule mzunguko wakati BWEGE [emoji2957] anautafuta ili auguse tu mpira [emoji460].

Mara nyingine BWEGE alikuwa anakimbiza mpaka anakata tamaa [emoji43] maana kuna wachezaji walikuwa na chenga za maudhi kabla ya kutoa pasi. Ukiwa BWEGE na hutumii akili utapigwa tobo au kanzu na kisha kusindikizwa na kofi la mgongoni [emoji23].

FUNZO: Kutafuta mpira wakati ukiwa kwa wapinzani (Marking)

Endeleza unayoijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…