Comrade Ally Maftah
Member
- Nov 6, 2016
- 77
- 271
WATENGE MARAFIKI KATIKA MAKUNDI
Na Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
Kutokana na utafiti nilioufanya katika miaka yangu 32 niliyoishi duniani, nimejifunza kuweka marafiki katika makundi mane ( 4 ).
1. DIAMOND FRIENDS(PLATNUMS)
Hawa ni wale marafiki ambao wanakupenda wewe moja kwa moja bila kuzingatia chochote kutoka nje ya wewe, sifa ya hawa marafiki huwa hawafuatilii unapokosea na wanachukua tahadhari kubwa pindi wanapotaka kukushauri jambo, na ziada ya hapo huwa hawaingilii uhuru wa maisha yako.
2. GOLD FRIENDS (AURUM )
Hawa ni wale marafiki ambao upo nao na wanakupenda kwa wakati huo, ila ikitokea kuna jambo limejitokeza kuhusu wewe wanaweza kubadili mawazo, hasa wakikutana na watu wanaokuchukia wanaweza kuungana nao, ila kwa wakati huu ni marafiki wazuri, sifa ya hawa huwa hawachukui tahadhari yoyote pindi wanapotaka kukukosoa, kukushauri, na hawa huwa ni wepesi kuingilia uhuru wa maisha yako.
3. SILVER FRIENDS(ARGENTUM)
Hawa ni wale marafiki ambao hawana muda kabisa na wewe, kwa lugha nyepesi ni kwamba hawakupendi na hawakuchukii wao wapo kwenye msawaza kuhusu wewe, hawa unatakiwa kuchukua tahadhari katika kuishi nao, kwa sababu kuna uwepesi mkubwa wa kuwa maadui wako, hawa ukikosea huwa hawachelewi kukushikia bango, ukiwa sawa pia hukushangilia.
4. IRON FRIENDS
Hawa ni watu wenye chuki na wewe, kifupi ni kwamba ni maadui zako wao huwa hawaoni jema unalolifanya, ukifanya jema wanajifumba macho na wanachukia wao wanasubiri ukosee wakubebee bango, marafiki wa hivi unatakiwa kuchukua tahadhari kubwa sana katika kuishi nao, unatakiwa kuwaficha sana hatua za maendeleo yako, hawa ni watu hatari zaidi kwenye maisha,
ZINGATIO
Marafiki hawa hubadilika kwa mtu na mtu, anayeweza kuwa gold kwako, kwa mwenzako anaweza kuwa silver au diamond, isipokuwa hawa iron, huwa wanakuwa iron kwa watu wengi hawa ni wale watu walioumbwa na mioyo iliyojaa chuki, hawapendi kuona mtu yoyote anakuwa na furaha.
Unatakiwa kujifunza kuishi nao wote kwa sababu kila rafiki ana kitu cha kukupa, hata hawa iron kuna wakati tunawahitaji sana.
Nilichoandika na mawazo yangu, hayahusiani na mapitio ya watu wengine hivyo kama una wazo mbadala na wewe kama una fikra andika kwa upana.
Ndimi Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
RAFIKI WA WOTE