Kanzi data itayounganisha hospitali zote za umma na binafsi ni jambo la muhimu

Kanzi data itayounganisha hospitali zote za umma na binafsi ni jambo la muhimu

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,647
Reaction score
9,604
Duniani kumekuwa na magonjwa mengi na matibabu yake yamekuwa complicated kidogo, mengine yanahitaji historia ya mgonjwa ili kuweza kumtibu na mengine yapo complicated kiasi unaweza kutibiwa hospitali 4 na ile ya nne ndo ukapata tiba sahihi.

Mwezi wa 7,2020 nilimpeleka mjomba wangu hospitali fulani baada ya kumwona Daktari , Daktari aliomba apelekewe taarifa za awali alizopata matibabu kabla ya kumtibu basi tukafanya mchakato zikapatikana baada ya siku 3 akaanza matibabu mapya ambayo yalipelekea ahueni kubwa na tunatagemea hali ikiendelea vizur atapona kabisa.

Katika kuongea na yule Daktari alituambia kama angeamua kufuata maelezo yetu bila kujua dawa alizopata awali kuna uwezekano mkubwa angefariki maana dawa alizotumia awali na alizotaka kumpa reaction yake ni mbaya sana.

It means huyu Daktari anajua kazi yake, vip tungekutana na Daktari ambaye anajali fedha tuu mambo yangekua mabaya zaidi.

Ombi langu kuwe na DATABASE nchi nzima ambayo hospitali za umma na za binafsi kiasi mgonjwa akienda hospitali yoyote iliyosajiliwa Daktari au wahudumu wa afya wanaweza kupata taarifa zake zote za ugonjwa bila ya kumwuliza mgonjwa kwa kua sio wote waoaweza kujieleza kwa ufasaha na sio wote wana kumbukumbu sahihi. ..

Mtaji wako Afya yako.
 
Umesema kweli hili suala ni muhimu sana.

Me kuna kipindi nilikuwa naumwa nikaenda hospitali mara ya kwanza nikapimwa damu nikakutwa na malaria, nikapatiwa dawa.

Baada ya siku kadhaa hali ya ugonjwa ikarudi tena, nikaenda hospitali ileile nikamkuta daktari mwingine, naye akanambia nikapime tena kipimo kilekile cha mwazo, nikamwambia hicho kipimo nimepima Siku kadhaa zilizo pita, akanambia Mimi ndio daktari nakwambia ukapime.

Nikaenda kupima sikukutwa na tatizo lolote lakini nilikuwa naumwa, basi akinihoji zaidi kisha akaniandikia dawa, nikatumia nikapona.

Sasa kama kungekuwa na data base basi angeendelea pale nilipoishia na si kuanza upya. Ni usumbufu.
 
Hili linawezekana sema shids kubwa ni kuhakikisha usalama wa taarifa za mgonjwa na miundombinu ya kuwezesha hilo suala.
Taarifa zitalindwa kwa wataalafu wa afya kulinda taarifa za wagonjwa maana hata sasa kuna taarifa nyingi za wagonjwa na zipo salama.
 
Umesema kweli hili suala ni muhimu sana.

Me kuna kipindi nilikuwa naumwa nikaenda hospitali mara ya kwanza nikapimwa damu nikakutwa na malaria, nikapatiwa dawa.

Baada ya siku kadhaa hali ya ugonjwa ikarudi tena, nikaenda hospitali ileile nikamkuta daktari mwingine, naye akanambia nikapime tena kipimo kilekile cha mwazo, nikamwambia hicho kipimo nimepima Siku kadhaa zilizo pita, akanambia Mimi ndio daktari nakwambia ukapime.

Nikaenda kupima sikukutwa na tatizo lolote lakini nilikuwa naumwa, basi akinihoji zaidi kisha akaniandikia dawa, nikatumia nikapona.

Sasa kama kungekuwa na data base basi angeendelea pale nilipoishia na si kuanza upya. Ni usumbufu.
Kweli sana maana kuna wagonjwa wanaugua gafla wakifikishwa hosptal baada ya matibabu kidogo unasikia wamefariki... labda unaweza kuta yule mgonjwa alikua na matibabu anafanya kabla na gafla anabadilishiwa kitu kinachopelekea kifo chake. Pangekua na database ni rahisi kujua kama mgonjwa alikua anatumia dawa za ugonjwa flani hivyo kumpa matibabu stahiki
 
Ni kweli, unaweka fingerprint na data zako zote za miaka yote zinaanikwa live bila chenga
 
Ni kweli, unaweka fingerprint na data zako zote za miaka yote zinaanikwa live bila chenga
Itasaidia sana kujua holistoria ya afya ya mgonjwa bila haja ya kuuliza maana sio wote wana kumbukumbu sahihi za ugonjwa wa miaka mingi iliyopita
 
Back
Top Bottom