SoC02 Kaondoka pedeshee katuachia mchunaji

SoC02 Kaondoka pedeshee katuachia mchunaji

Stories of Change - 2022 Competition

Bosi Kalewa

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
7
Reaction score
4
Dingii alikuwa mshua ambaye life style yake ilikuwa ya Kipedeshee. Wale madingi hongahonga wa mjini. Ambao huingiza milioni moja na kuhonga laki tisa nzima. Hata hajutii!

Alipokuta mkwanja mwingi umekaa tu pale Hazina. Kwanza akashangaa. Na ndo hapo msemo wa "Sisi ni matajiri sana". Ukaanza kuvuma kwa kasi kutoka katika kinywa cha Dingii. Alipagawa.

Alikuta pesa nyingi kuliko zile zilizopo katika akaunti yake. Kwenye Wizara yake au chumbani kwake. Ndo stori na maelezo ya sisi ni matajiri sana tusidanganywe yakawa hoti. Kumbe Dingii kadata.

Minoti ilimpagawisha na kutangaza ghafla ununuzi wa ndege. Tena kwa keshi na siyo kuungaunga! Ndege zaidi ya 10 akalipia jumla jumla akisubiri zije. Tripu za Airport kuzipokea kwa mapambio zikaanza.

Bado akaona pesa ipo ya kutosha hazina. Akajisemea moyoni "Usinitanie wacha nitimize ndoto ya Baba wa Taifa." Ghafla akaamuru serikali yote iende Dodoma. Kisisalie kitu Daslama mjini.

Ununuzi wa ndege kipedeshee, serikali kupelekwa Dom kibabe. Miradi mingi ya sifasifa kama karavati za Ubungo na Tazara. Eti wanaita 'flaiova'. Ili ujue zile ni karavati ziizopandiana kacheki ramani ya awali.

Uwanja wa ndege usio na tija kule bushi kwake. Kubeba pundamilia, ngedere na nyumbu kupeleka bushi kwake. Kujenga majengo mengi bushi kwake. Pesa zote zikakata jumla.

Wenzake walihamishia serikali Dodoma hatua kwa hatua. Walijua ni gharama sana. Na ndege hazinunuliwi kwa keshi hata kwa taifa kubwa kama Marekani. Dingii alileta upedeshee hapa.

Mkwanja ulipokata akaanza kukopakopa kinyemela. Kwa miaka mitano tu alikopa zaidi ya watangulizi wake. Huku akitufunga kamba kuwa; "Tunajenga kwa pesa zetu wenyewe." Ujue alitufanya mabwege.

Achana na ununuzi wa wapinzani wake. Kutapanya pesa kila alikopita na misafara ya kibedui. Iliyojaa ghiriba, kamera nyingi na msululu wa gari za kifahari. Mikwanja ikaisha.

Mshua akasepa kurudi zake mbele za haki kwa Mungu Baba Mwenyezi. Huku nyuma akituachia kapu tupu pale hazina. Kifupi Bi Mkubwa kakuta zigo limekata lote. Ndo maana akaja na mishe za tozo.

Bi Mkubwa kalazimika kutuchuna wanae kwa tozo. Huku akiweka sawa uhusiano na 'Madon' wa mbelembele ili nao awachune aje kutulisha. Dingii alitibuana na weupe wenye mawe akiwaita mabeberu.

Hata angekuwa ni Julius! Hali aliyoacha Dingii, naye angepata tabu kuliweka sawa taifa kwa muda mfupi. Tozo ni matokeo ya Upedeshee wa kutapanya pesa ovyo. Na kuacha patupu hazina.

Ni kwamba, tulikuwa na Dingii pedeshee. Kasepa na kutuachia Bi Mkubwa, ambaye sasa analazimika kutuchuna sisi na madon weupe wa huko duniani ili tuishi. Yes ndo ukweli.

Kasikilize ngoma ya Dingi ya Mandojo na Domo Kaya...
 
Upvote 0
Back
Top Bottom