Kapeti ipi inapendeza kukaa gheto

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Achana na hizo kapeti za mita elfu 7,kapeti zipi nzuri zinazopendeza kukaa gheto,
Yaani ile mtu akiingia gheto Aone kuna utofauti ajishuku ata kuingia na soksi miguuni.

Kesho nina mpango wa kununua kapeti niitandike gheto, niliyokuwa nayo imechakaa ila tatizo bado sijajua ni ipi inafaa,

Bajeti yangu ni 150k(laki moja na nusu),


Cc Zero iq
 
Upo Dar? Nenda Kariakoo Msimbazi au Mlimani City Discount Centre wanazo kali sana. Za manyoya (sio yale marefu).

Unachofanya kama huna tiles ghetto tanguliza lile la draft draft la mita 1 buku 7 then kwa juu unaleta ilo. Maana lenyewe halita cover chumba kizima.

Mimi nilichukua pia yale ya wall to wall (ya kukata) yenyewe urefu mita 1 kwa upana mita 3 yalikua elfu 30/35 nayo nikaweka sebuleni ya ukweli kinoma.

Mlimani city na K Koo bei ni sawa tu.

Ila kuna wajamaa pia wanauza pale Kariakoo nje ya Mobile Plazza maybe wanaweza kua na bei nafuu.
 
Hivi gheto ndo nini? Ni chumba cha kulala katika nyumba ya kupanga au? Kama ni nyumba yako weka zile tiles 70x70 zinazong'aa kama kioo hutajutia pesa yako na zinadumu miaka! Jinsi zilivyo na heshima wewe mwenyewe kukanyaga juu yake utajihisi hujazitendea haki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…