Kapita Bila Kupingwa - Mgombea Pekee

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kazimwaga zake sera, ilani kanipatia,
Kaniomba zangu kura, moyo kuuchagulia,
Imekuwa werawera, nia kanitangazia,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!


Bila ya kuchakachua, mgombea kajinadi
Ahadi nimechambua, nimeshindwa ukaidi,
Mwishoni nimeamua, ni mgombea stadi,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!

Kura nimempatia, asubiri kuapishwa,
Wengine wamekimbia, yeye pekee kapishwa,
Hongera nampatia, wote mtafurahishwa,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!!

By. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Mgombea Pekee!
 
Aisee huyu mtu ni mult-talented, big up mkubwa
 
huyo unayemsema, kagombea chama gani
ni CUF au CHADEMA, tujulisheni jamani
ni baba au ni mama, jamani niambeni
Kama kapita hakupingwa, sio mshindi wa kweli

sio mshindi wa kweli, naomba kusisitiza
hakushinda kwa adili, kitu hiki chatatiza
nani kachukua ya pili, kama yeye ni wa kwanza
ushindi wa bure bure, mimi siufagilii
 
Kazimwaga zake sera, ilani kanipatia,
Kaniomba zangu kura, moyo kuuchagulia,
Imekuwa werawera, nia kanitangazia,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!

Wastahili pongezi, wa kijiji nakwambia
Ni wazi umemuenzi, sera zake kutambia
Aliupanga utenzi, kura zako kuomnea
Umechagua sawia, Mgombea anofaa


 
Hongera malenga wetu niko kwenye kitendawili ,sijaelewa maana
 
Huyo ni laurence masha. Dhana ya mzee mwanakijiji hapa nilivyomuelewa mimi ni kwamba, hakuna mgombea hata mmoja aliyepita bila kupingwa, maana wananchi hawakuulizwa kama wanawahitaji au hapana, ilitakuwa kuwe na visanduku vya ndio au hapana, msingeamini masikio yenu, labda nusu yao wangekatariwa na wananchi. Mfano mdogo jimbo la prof anna tibaijuka yeye amepita dezo dezo, lakini chadema imepata madiwani 8 na ccm imeambulia madiwani 3. Je wananchi hao wangepewa nafasi ya kupiga ndio au hapana ingekuwaje? Tafakali.
 
Fumbo hilo ni zito lahitaji muda kulitafakari.....vinginevyo utachakachua majawabu yake.................
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…