Kapombe na Zimbwe ndio watakao mfukuzisha kazi kocha Fadlu

Kapombe na Zimbwe ndio watakao mfukuzisha kazi kocha Fadlu

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
Hawa wawili ni full backs Bora kabisa kuwahi kutoka hapa Tanzania ( ila tukubaliane kazi na umri shehe )

Wametumika na makocha wengi kwa mda mrefu na Bado wanaendelea kutumika ( hili ndilo AMBALO Mimi nalikataa na nitalipinga daima )

Just imagine, kwenye mechi za kimataifa ni wao, NBC wao, fa Bado wao.....watafanyiwa sub kipindi Cha pili pale TU timu ishapata matokeo kweli??

Nyie mashabiki wa Simba kuanzia hapa JF na kote duniani hili hamlioni?

Kwanini Hawa wachezaji hawapumzishwi??, mara nyingi sana wanacheza under performance ni vile saidia Mungu TU tunapata matokeo

Nyie mashabiki wenzangu acheni umandazi, acheni kukariri namba 2,3 ni wao TU Ata wacheze under performance mnakaa kimya TU,

Kocha fadlu, mbona mara nyingi akicheza Valentin Nouma kwenye fullback ya kushoto anacheza hizo dakika chache lakini michango wake ni mkubwa hasa kwenye kutengeneza nafasi kuzidi zimbwe?

Hii game plan Yako ya kuwatumia kapombe, zimbwe ku overlap nakuhakikishia itakuondoa Simba, nipo paleee nimekaa
 
Kuna ,timu ya simba na man united izo timu za kijinga sana miaka hii ,,ukizifuatilia chanzo chake viongozi nilizipuuza baada ya kuona viongozi wenyewe hawataki ziendelee
 
Kwa mtizamo wangu Kapombe amekuwa msaada sana hasa anapopanda mbele kusaidia mashambulizi pasi zake na krosi zake zimekuwa na usahihi mkubwa sana mtaani wanasema zina macho. Ila kwa Zimbwe sijui kakumbwa na nini sijui ndo ufadha wenyewe. Anakaba vizuri anapanda vizuri lakini inapofika kwenye kupiga krosi hata kama yupo kwenye kibendera cha kona na washambuliaji wanasubiri mpira katikati utaona yeye huyo anaanza kurudisha mpira nyuma. Na haya mapungufu ya Zimbwe hakuwa nayo mwanzoni na mbaya zaidi sio mashabiki wengi wa mpira wanayaona.

Na wachezaji watakaomfukuzisha Fadlu Simba ni Che Malone, Mutale na Mukwala. Che Malone sasa hivi kila mechi lazima atoe maboko mawili mpaka matatu lakini timu pinzani hazijaweza kuzitumia vyema. Mutale hamna mchezaji pale lakini anachezeshwa kwa sababu inaonekana kuna viongozi wanampenda na benchi la ufundi linampenda ila itaendela kuwagharimu sana Simba kadiri wanavyolazimisha kumtumia. Mukwala huyo ndio kabisa Ateba akiwa hayupo huyo hana msaada wowote kwenye timu zaidi ya mikimbio mizuri tu uwanjani kama alivyo mwenzake Mutale.
 
Mtajua wenyewe sis tunachojua kocha Ong Bak ni mwalimu bora sana wa karate..
 
sisi kama makolo tutahakikisha tunacheza shirikisho tena mwakani na hakuna wa kutupangia,shwain!
 
Zimbwe nilishamkataa since simba ile ya 2019/2020....huyu jamaa ni mbovu na ana mpira wa kizamani. Utakuta winga anapanda na mpira yeye kabaki nyuma, Hawezi kupiga Cross wala V-passes pindi anapoingia kwenye box, pia huwa hana nguvu wa kupiga mashuti na mguu wake wa kushoto.

Ni vile tu amepachikwa jina kuuuuuubwa Shabalala.

Matatizo ya Shabalala ndio hayohayo aliyo nayo kapombe halafu pia hawana kasi. Katika Modern Football ambapo fullbacks zinacheza kama wingbacks au inverted midfielders hawa jamaa hawawezi kabisa roles hizo. Wameshazoea kucheza kama fullbacks wa 1990's kaa nyuma subiri wapinzani waje ukabe...ndio mpira wao huo.

Falsafa ya fadlu ni ngumu kuendana nayo..inahitaji wachezaji wenye kasi. sana
 
Muendelee kushutumiana hivi hivi ili siku ikifika, mnyama achinjwe mapema! tunywe supu.
 
Hawa wawili ni full backs Bora kabisa kuwahi kutoka hapa Tanzania ( ila tukubaliane kazi na umri shehe )

Wametumika na makocha wengi kwa mda mrefu na Bado wanaendelea kutumika ( hili ndilo AMBALO Mimi nalikataa na nitalipinga daima )

Just imagine, kwenye mechi za kimataifa ni wao, NBC wao, fa Bado wao.....watafanyiwa sub kipindi Cha pili pale TU timu ishapata matokeo kweli??

Nyie mashabiki wa Simba kuanzia hapa JF na kote duniani hili hamlioni?

Kwanini Hawa wachezaji hawapumzishwi??, mara nyingi sana wanacheza under performance ni vile saidia Mungu TU tunapata matokeo

Nyie mashabiki wenzangu acheni umandazi, acheni kukariri namba 2,3 ni wao TU Ata wacheze under performance mnakaa kimya TU,

Kocha fadlu, mbona mara nyingi akicheza Valentin Nouma kwenye fullback ya kushoto anacheza hizo dakika chache lakini michango wake ni mkubwa hasa kwenye kutengeneza nafasi kuzidi zimbwe?

Hii game plan Yako ya kuwatumia kapombe, zimbwe ku overlap nakuhakikishia itakuondoa Simba, nipo paleee nimekaa
Mmeanza kelele, lakini wachezaji bora kwa Simba msimu huu ni Kapombe na Shabalala. Jamani sare tu imewachanganya, tutasikia mapambio yote.
 
Washapumzika sasa......Sema Kingine.!

Kuwafananisha hao na kina Yao na Kibwana Shomari waliopokwa namba na Mwenda mshaacha?
 
Wewe kaa tu hapo unaposema, eti hao ni full backs wazuri kuwahi kutokea katika Tanzania..!!! Nafikiri wewe utakuwa umezaliwa kwenye miaka ya tisini na kitu.

Hao ndio full backs wabovu kuwahi kutokea katika Tanzania, hiyo ndio tathmini yangu kwa sisi tuliyo waona akina Mohamed Ali Chuma, Mohammed Kajole (Machela), Ahmed Amasha, Samli Ayub, Hussein Kondo (Mmakonde) John Faya, Zakaria Kinanda, Shaaban Baraza, Juma Shabani, Daudi Salum (Bruce Lee), Rajab Digongwa, Yusuf Bana, Mohammed Hashim (Mkweche) nk.

Hao walikuwa ni full backs wa kutolea mfano na walikuwa na mapafu kama ya mbwa wakipanda na kushuka kwa kasi ileile kwa dakika tisini zote za mchezo huku wakimimina krosi za hatari.
 
Back
Top Bottom