Huyu anafaa alaniwe ni adui wa Taifa hili la Tanzania , hata sijui kama linafahamu kuwa nchi imevamiwa na mafisadi ? Kama kuna mawaziri wanapuliza basi huyu ni mmojawao yaani mambo ya kiCCM kukurupuka tu,yule mmoja kaulizwa kasema Zanzibar si nchi Nyerere na ujuaji wake wote hajawahi kutamka hivyo ,eti katiba ,hivi Katiba inasema nini juu ya watu wa dizaini ya mafisadi WaTz tunataka muheshimiwa Pinda atamke na ailinde katiba kama kweli anafuata na kuyaheshimu yalio ndani ya Katiba.
halafu huyu waziri aliesema mambo ya wimbo ivi ana akili timamu huyu ,au ndio wanaosaboteji utawala wa Mh.Kikwete kwa kuzusha mambo ambayo yataleta na kuonyesha kama serikali imejaa mambumbu na hivyo moja kwa moja kumlengesha Mheshimiwa Kikwete ,inawezekana kabisa haya ni mambo ya mtandano unaokwenda agaist our Leaders who are trying to their best to keep the country on the track again ,wanafanya kila mbinu alimradi kuharibu ,huyu ni Waziri katika Serikali anakwenda kusema upuuzi kama huu,kama sio saboteji ni kitu gani ? Kitu kidogo tu kinaweza kuivuruga akili ya watu kwa serikali yao na kuiona haina maana,na ndivyo wanavyofanya ,wanachokonoa mambo hayana hata maana , raisi anafaa kuwaangalia watu kama hawa na kuwatenga ikibidi awaondoe mara moja wakatafute shamba walime.
Hata watu wa dini hawajakataza mamboya dini kuwekewa kwenye mobile phones ,ila linazuka jitu hili ambalo eti ana wazifa wa Uwaziri anakwenda kuonya na kutoa tahazari wimbo wa Taifa ni marufuku kuwekwa kwenye phones,eti inawezekana simu ikaita na mziki huo ukawa unaimbwa na simu hiyo sehemu isiyokuwa tohara,hiyo ndio maana yake huwezi kuleta maana nyingine zaidi ya hiyo ,pengine mtu huyu ukimpa filimbi aupige wimbo wa Taifa hawezi atabakia kurusha mate tu ?
Halafu eti amekuwa mtetezi wa kufika kutamka aliyotamka kama si fisadi huyu ni nani ,wanasaboteji na kuipa serikali wakati mgumu sana kwa mambo ya kipuuzi puuzi kama haya,sasa watu baada ya kujadili maendeleo anajadili mambo ambayo hayana kichwa wala miguu ,hiyo wizara yake imeoza inatafuna fedha kwa kuwalipa makocha wa kigeni na hakuna kinachoonekana si ajabu kama mgao mwengine unaingia mfukoni,watu wanaojipendekeza kiaina ni hatari kwa uchumi wa Taifa.