Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amezindua kiwanda cha kusindika nyanya kilichopo katika mji wa Bobo-Dioulasso.
Uzinduzi wa kiwanda hicho umefanyika leo tarehe 30 Novemba 2024 . Kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchakata tani 6 za nyanya kwa saa moja, kinatazamiwa kuiwezesha nchi hiyo ya Afrika magharibi kukabiliana na tatizo la upotevu mkubwa wa nyanya baada ya mavuno uliotokana na ukosefu wa kiwanda cha kusindika zao hilo.
Fedha za kujenga kiwanda hicho zilitolewa na wananchi wa Burkina Faso kupitia mpango wa ununuzi wa hisa uliowezesha hata wananchi wa kipato cha chini kuwa sehemu ya umiliki wa kiwanda hicho.
Viwanda vingine viwili kama hicho vinajengwa katika miji mingine na vinatarajiwa kuwa tayari kuanza uzalishaji hapo mwakani.
Nchi ya Burkina Faso ni ya pili kwa uzalishaji wa nyanya katika nchi za Afrika magharibi nyuma ya Nigeria na huuza nyanya nje ya nchi hasa katika nchi za Bénin na Ghana.
Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi, Kapteni Traore aliwashukuru raia wa Burkina Faso kwa kuitikia mpango wa ununuzi wa hisa uliowezesha kupatikana kwa fedha zilizowezesha ujenzi wa kiwanda hicho ambacho ni alama ya maono waliyonayo ya kuwezesha upatikanaji wa maendeleo kwa raia wote wa Burkina Faso.Pia alisema kwamba anaamini nchi ya Burkina Faso ina raslimali muhimu zinazohitajika ili kuiletea usitawi na maendeleo nchi hiyo.
CHANZO/ SOURCE:Shirika la habari la Burkina Faso (RTB)