Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza tarehe 18 Oktoba, 2024 Amejiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kiwanda.
Mbunge Juliana Daniel Shonza amefanya ziara ya kupita Mtaa kwa Mtaa kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika siku chache zilizosalia lililoanza tarehe 11 - 20 Oktoba, 2024 ili kujihakikishia haki ya kupiga kura kipindi cha uchaguzi, 27 Novemba, 2024.
Aidha, Juliana Daniel Shonza katika ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa ameambatana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Songwe, Bi. Emeliana Mwakyoma pamoja na viongozi mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaenda kujiandikisha na kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024
Shonza amesema lengo la kuhamasisha watu kujiandikisha ni muendelezo wa kujipanga haswaaa na kuhakikisha Kapu la Kura za Mama Samia Linajaa Mapema Katika Mkoa wa Songwe na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashinda Mitaa, Vijiji na Vitongoji.