SoC02 Kapungu

Stories of Change - 2022 Competition

Actuality

Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
7
Reaction score
10
MANDONGA

UTANGULIZI

Katikati ya kiwanja inapigwa pasi mpenyezo anakutana nayo mchezaji wa Insta united ambae ni namba tisa tishio, anapiga shuti kali ambalo uwanja mzima uliamini ni goli, anajitokeza golikipa kama nyani anaruka na kudaka mpira ule moja kwa moja huku kwetu tunaita kaumeza wote. Hata aliepiga mpira ule haamini kama kipa kaudaka, uwanja mzima watu wanapiga makofi, na kushangilia. Unaweza kudhani huyo aliedaka ni bonge moja la mtu, mwenye mwili mkubwa sana, hapana ni kijana mdogo tu anaesoma katika shule ya sekondari Juhudi kidato cha tatu anaitwa Kareem MANDONGA mwenye umri wa miaka 17 na urefu wa karibia sentimeta 164. Jina la Kareem hata watu hawalijui wao wanajua jina la baba yake tu MANDONGA ambalo ndio watu wengi wanajua ni jina lake.

ENDELEA

Mech ile ilikuwa kama ni ufunguo wa maisha ya soka ya Mandonga. Akapata bahati ya kukutana na askari jeshi aliekuwa mapumzikoni kijijini kwao Songambele ambaye alikuwa ni mchezaji wa timu ya jeshi, iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza. Askari huyo hata yeye uwanja huo huo ndio uliyomfanya akapata uaskari wake na kuwa mchezaji wa timu ya jeshi. Baada ya mchezo alipomuona Mandonga ili kumsalimia akamfuata Mazungumzo yakawa kama ifuatavyo

Mjeshi: Dogo niaje

Mandonga: Safi tu kaka shikamoo

Mjeshi: Marhaba nimeona mambo yako si mchezo. Wewe ni golikipa mzuri sana, fanya mazoezi sana una kipaji kikubwa mdogo angu utafika mbali sana

Mandonga: Hahahahahahaa kawaida tu kaka.

Mjeshi: Sio kawaida mdogo wangu unachofanya makipa wengi hawawezi.

Mandonga: Sawa kaka nashukuru sana. Natamani siku moja niwe kama wewe

Mjeshi: Pambana uwe zaidi yangu kwani Manula anakuzidi nini??

Mandonga: Ahhahahahaha kaka huko mbali sana kaka

Mjeshi: Unaweza kikubwa wewe pambana sana na ufanye mazoezi sana utafanikiwa ila nidhamu kwa mchezaji ni muhimu sana

Mandonga: Sawa kaka nashukuru sana

Wakaachanana maisha yakaendelea kama kawaida. Mandonga akaendelea kuwa maarufu kijijini kwao kwa kuwa golikipa bora zaidi alipendwa na watoto na wakubwa, wazee na kina mama.

Hakika mpira ulimpa sifa nyingi sana na akatambulika kila mahali kwa kipaji chake. Kuna kipindi alikuwa hadi akichangiwa hela ya matumizi na mashabiki kila baada ya mchezo kumalizika, na akaitumia hela hiyo kutamba nayo shuleni. Aliendelea na masomo hadi siku moja baba yake alipopokea simu toka kwa kocha wa timu ya jeshi (JKT) akitaka wamchukue kijana wake akajiunge na timu, baba yake Mandonga hakuuwa na shida na tatizo na hilo. Mandonga aliporudi toka shule baba akamuita kwa mazungumzo

Baba: Kareem?

Mandonga: Naam Baba

Baba: Njoo sebuleni mwambie na mama yako aje nina mazungumzo na nyie wawili

Mandonga: sawa, mamaaa njoo huku baba anakuita.

Kikao cha familia cha watu watatu

Baba: Mama Kareem, leo nimepokea simu kutoka hukoo jeshini JKT wameomba Kareem akajiunge na timu yao ya jeshi, kwa sasa atacheza tu katika timu za vijana ila akitimiza miaka 18 atapewa mkataba wa kuchezea timu kubwa nayo ni mwakani sio mbali sana.

Mama: Na shule je anaacha?

Baba: Hapana ataendelea na shule huko huko

Mama: Sawa kama ni hivyo mungu amtangulie mwanangu ukapambane uajiliwe uwe mwanajeshi mwanangu. Ila shule ndio msingi wako wa kila kitu cheza mpira ila usisahau shule mwanangu.

Mandonga: sawa mama na baba nitajitahidi kwa uwezo na kipaji changu

Baba: wewe ni mwanaume mwanangu sitegemei ushindwe maisha ya jeshi, natumaini utayaweza yote katika yeye, wakasali pale kwa kumbariki kijana wao.

Baaada ya siku tatu Mandonga akaanza safari ya kuelekea jeshini kuanza maisha mapya na ya uhakika. Vijana wengi mtaani walimtamani sana Mandonga na wengi wakatamani nafasi aliyopata wangepata wao na hivyo ikaongeza chachu vijana mtaani kupambana ili waonekane waweze kutoka na kufika mbali kama ilivyo kwa Mandonga. Lakini kumbuka Mandonga hakuaga shule, walimu wakawa wanasikia habari tu, na yeye akawa kama mtoro tu wa shule.

Huko alipoenda Mandonga akadanganya kamaliza shule hivyo hakuendelea na shule kabisa akawa anacheza mpira tu na shule akaacha jumla.

Mwaka umekata sasa Mandonga inafahamika ndio mwaka wake wa kupata mkataba wake awe mchezaji rasmi wa timu ya wakubwa lakini pia apewe nafasi ya kupitia mafunzo ya jeshi ili apate ajira mbali na mpira. Viongozi wa timu wakamuita mezani, ili wakae nae wampe mahitaji yao ya mkataba.

Moja ya mahitaji waliomba kwa Mandonga, ni cheti cha kuzaliwa na cheti cha kumaliza kidato cha nne. Hapo ndo mtihani ulipoanza kwa Mandonga, cheti cha kidato cha nne hana, cha kuzaliwa hana, ila tatizo kubwa ni cha kidato cha nne.

Ikabidi aseme ukweli tu, basi akapewa nafasi tena asome shule za jeshi arudie kidato cha pili, Mandonga akaona hali ngumu na kusoma hataki tena anataka hela.

Huko shule akasumbua sana ikabidi arudishwe nyumbani aje asome, nako tayari ashakuwa mtu maarufu hivo akaona kama kwenda shule ni kujishusha sana, na tayari ashatoka watu wanajua yeye ni mchezaji wa timu ya jeshi, hafu wamuone anaenda shule tena akaona ni kama aibu kwake, akaamua kuacha kabisa shule.

Nidhamu yake ikashuka sana akawa kila akishauriwa hasikii wala haambiliki,basi kwa kukosa vigezo timu yake ya jeshi ikamuacha akakosa timu na ajira jeshini kisa cheti cha kidato cha nne. Mandonga saivi anacheza ndondo tu mtaani anaingiza elfu tano, elfu 2 ya kula kwa siku za mechi.

Mandonga kwa sasa ni yatima hana baba wala mama wote wametangulia mbele za haki kwa ajali ya gari ambapo wazazi wake wote wawili walifariki kwenye ajali, yeye ndo kaka wa familia ndio mkubwa wadogo zake wanamtegemea yeye. Mandonga anajuta sana ukikutana naye anajutia sana nafasi alizopewa za kusoma na ajira akachezea kisa umaarufu mdogo tu wa utotoni, sasa anapiga mizinga tu watu na kazi ngumu kufanya hataki. Bado tunamsisitiza kila tukikutana nae Eeeehhh MANDONGA WEWE RUDI SHULE.
 
Upvote 6
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…