Kapuya ni nani kwenye hii nchi hadi awe juu ya Sheria?

Joyce Kiria

Member
Joined
Aug 6, 2013
Posts
50
Reaction score
109
Kilewo wangu ametafutwa kwa udi na uvumba na Jeshi la Polisi kwa sababu ya Taarifa za magazeti..

Kapuya kafunguliwa Jalada la tuhuma zinazoendelea kuvuma kwenye vyombo vya habari, kama haitoshi tuhuma zimefunguliwa na mlalamikaji ambae ana ushaidi kwa kiasi kikubwa, na hayo mambo yamedumu kwa muda sasa kwenye vyombo vya habari! Lakini jeshi la polisi halijashughulika nae!

Au ndo mambo ya kukamata wezi wa kuku na kuwajaza magerezani huku wanaomaliza nchi (mafisadi) wanakula Kuku uraiani?

Ama kweli hii ni Tanzania zaidi ya uijuavyo.. Tunawangoja kwa hamu sana 2015..

Kilewo Mume wangu nipo na wewe tena nipo Imara sana kuliko unavyonijua. Pigania nchi kitaeleweka tu.
 
Attachments

  • 20131129_081947.jpg
    20131129_081947.jpg
    610.5 KB · Views: 638
  • 20131129_083939.jpg
    20131129_083939.jpg
    767.2 KB · Views: 606
CCM wamejiweka kuwa untouchable Dada, wako juu ya sheria hata yeye alisema kuwa watoto wao wanauza unga lakini hamna wa kuwafanya kitu. Ipo siku upepo utabadilika.
 
kweli Tanzagiza ni zaidi ya uijuavyo.......Dada joy tuko pamoja na wewe mtafute yule binti wa Kapuya Ufanye nae mahojiano katika Wanawake Live ILI Jamii kubwa ione maovu yanayofanywa na viongozi wetu hafu bado wapo mtaani wanapeta tu
 
Issue ya mmeo na Kapuya ni tofauti,kwanza mmeo mwenyewe anamchukia Zitto waziwazi na aliandika humu JF,na hata akapost waraka unaomchafua Zitto,Kapuya je una ushahidi wowote kuwa alibaka kweli?Zaidi ya maneno tu?
 
Kilewo wangu ametafutwa kwa udi na uvumba na Jeshi la Polisi kwa sababu ya Taarifa za magazeti..

Kapuya kafunguliwa Jalada la tuhuma zinazoendelea kuvuma kwenye vyombo vya habari, kama haitoshi tuhuma zimefunguliwa na mlalamikaji ambae ana ushaidi kwa kiasi kikubwa, na hayo mambo yamedumu kwa muda sasa kwenye vyombo vya habari! Lakini jeshi la polisi halijashughulika nae!

Au ndo mambo ya kukamata wezi wa kuku na kuwajaza magerezani huku wanaomaliza nchi (mafisadi) wanakula Kuku uraiani?

Ama kweli hii ni Tanzania zaidi ya uijuavyo.. Tunawangoja kwa hamu sana 2015..

Kilewo Mume wangu nipo na wewe tena nipo Imara sana kuliko unavyonijua. Pigania nchi kitaeleweka tu.

Kapuya ni mwanachama Mwandamizi wa CCM, Hivyo kumkamata itakitia doa chama. Kwa haya mambo yetu Watanzania hasa dola ufanya upuuzi wa wazi wazi huu ndo maana Hata Kenyata jana hajasita kututukania Rais wetu kwamba alichohutubia Bunge mwezi uliopita ni upuuzi tu.
 
Joyce Kiria , Pole sana maana ukiishi na mwanaharakati lazima ukubali misukosuko.Kapuya issue yake imefikia mahali inaonekana kama imesusiwa na jamii pamoja na wanahabari wengine maana inaandikwa na Tanzania Daima tu.

Sifahamu kwanini hili swala limepewa uzito mdogo na vyombo vingine vya habari pamoja na mtoto kutoa taarifa Polisi rasmi lakini hatuoni juhudi za vyombo vya habari kupata ukweli wa hili.

Binafsi kama ikigundulika yule mtoto alifanyiwa hayo aliyosema nitalaumu jamii nzima na vyombo vya habari juu ya hili maana kama kulikuwa na ulaghai ilikuwa kazi yao kutafuta ukweli hasa issue yenyewe ikihusisha mtoto na mtu mzito kama Kapuya.

Binafsi najitahidi kuifuatilia kuona mwisho wake.
 
Last edited by a moderator:
kweli Tanzagiza ni zaidi ya uijuavyo.......Dada joy tuko pamoja na wewe mtafute yule binti wa Kapuya Ufanye nae mahojiano katika Wanawake Live ILI Jamii kubwa ione maovu yanayofanywa na viongozi wetu hafu bado wapo mtaani wanapeta tu

Alafu arushe kwenye TV ya nani?
 
Issue ya mmeo na Kapuya ni tofauti,kwanza mmeo mwenyewe anamchukia Zitto waziwazi na aliandika humu JF,na hata akapost waraka unaomchafua Zitto,Kapuya je una ushahidi wowote kuwa alibaka kweli?Zaidi ya maneno tu?

Issue ya Kapuya bila kujali ukweli ama uongo lakini issue nzima ina maswali mengi yanayohitaji majibu.Kuanzia matumizi ya simu yake kwa vitisho na maneno yaliyotumika mazito sana.Kwanini Polisi wameshindwa kuchukua hatua haraka ili uongo na ukweli uwe wazi?
 
Issue ya mmeo na Kapuya ni tofauti,kwanza mmeo mwenyewe anamchukia Zitto waziwazi na aliandika humu JF,na hata akapost waraka unaomchafua Zitto,Kapuya je una ushahidi wowote kuwa alibaka kweli?Zaidi ya maneno tu?

Hivi wewe ni mwanamke kweli,unajua violence against women ?
Hujui kuwa wanaume wengi wanatumia kipato/vyeo kufanya mambo kama haya?
 
Uko kumtetea mmeo kwa gharama ya Kapuya? Conflict of interest, ungeweza kuipanga bila kuweka personal interest yako usoni ki hivyo.
 
Ila asimlishe maneno.

Nadhani mahaka ndio sehemu sahihi.

kweli Tanzagiza ni zaidi ya uijuavyo.......Dada joy tuko pamoja na wewe mtafute yule binti wa Kapuya Ufanye nae mahojiano katika Wanawake Live ILI Jamii kubwa ione maovu yanayofanywa na viongozi wetu hafu bado wapo mtaani wanapeta tu
 
Hivi wewe ni mwanamke kweli,unajua violence against women ?
Hujui kuwa wanaume wengi wanatumia kipato/vyeo kufanya mambo kama haya?

Huyo aliebakwa yupo wapi?kwa nini asijitokeze waziwazi na kusema polisi?au yeye mwenyewe akaongea waziwazi?mimi ndo nijitie kimbelembele?Kila siku tunasoma kwenye Tanzania daima kapuya alibaka.ushahidi hata kuwa labda wamekuta sperms wa huyo msichana hautolewi,zaidi ya maneno tu maneno.
 
Tena umenifumbua macho, gazeti la chama, anayelalamika hapa mke wa kiongozi wa chama.
Uji.nga mtupu
Huyo aliebakwa yupo wapi?kwa nini asijitokeze waziwazi na kusema polisi?au yeye mwenyewe akaongea waziwazi?mimi ndo nijitie kimbelembele?Kila siku tunasoma kwenye Tanzania daima kapuya alibaka.ushahidi hata kuwa labda wamekuta sperms wa huyo msichana hautolewi,zaidi ya maneno tu maneno.
 
Kapuya ni mwanachama Mwandamizi wa CCM, Hivyo kumkamata itakitia doa chama. Kwa haya mambo yetu Watanzania hasa dola ufanya upuuzi wa wazi wazi huu ndo maana Hata Kenyata jana hajasita kututukania Rais wetu kwamba alichohutubia Bunge mwezi uliopita ni upuuzi tu.

Huo ndio ukweli, TZ fupukeni macho muoni, tumieni bongo zenu kutafakari.
 
Back
Top Bottom