SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Katika mafanikio ya mchezaji, kuna kuujua mpira ila pia kuna bahati.
Bahati inaweza kukufanya upendwe hata kama mchango wako kwenye timu ni wa kawaida, bahati inaweza kukufanya upendwe na kila kocha, bahati inaweza kukufanya uwe unafunga mara kwa mara tena katika mechi kubwa, bahati inaweza kukuepusha na majeraha. Kinyume cha kuwa na bahati ni kinyume cha hayo niliyotolea mfano. Bahati ina nafasi yake katika maisha ya mchezaji.
Karabaka alikuja Simba na mpira wake wa kwanza tu kuugusa akiwa katika jezi ya Simba lilikuwa ni shuti lililoenda kuwa goli. Unahitaji mfano mwingine wa bahati?
Toka amesajiliwa Simba, Karabaka amefunga magoli mengi kumzidi Denis Kibu pamoja na kwamba Kibu kacheza mechi na dakika nyingi sana kumzidi na wanacheza nafasi moja.
Nilishangaa mechi ya ngao alipopangwa kucheza mechi nzima ila nilipokumbuka nyota yake sikushangaa tena. Yeye ndiye alifunga goli pekee lililoipa Simba medali.
Muite Bahati Karabaka.