Elections 2010 Karagwe: Matokeo kutangazwa?


Asante mkuu
 
HIVI KWANINI HII NCHI IMEGEUZWA NA WACHACHE KUWA KAMA ILIUMBWA KWA AJILI YAO....wanakaragwe jikazeni tunisheni misuli hiyo ni tishia nyau ni hadi kieleweke huko. Tupo pamoja
.
 
Habari kutoka Karagwe zinadokeza kuwa kuna ugumu wa kutangaza matokeo na sasa polisi wanataka kuongezwa katika jitihada za kuwatawanya mashabiki wa Deusdedit ambaye ametarajiwa kwa kiasi kikubwa kushinda. Ikumbukwe kama ilivyotokea Nyamagana huyu kijana alienguliwa na msimamizi wa uchaguzi mwanzoni, alichelewa kuanza kampeni lakini akarudishwa na Tume ya Uchaguzi.
 
Viongozi wa Chadema waongeze makada kusaidia jitihada za kulinda zoezi la kujumlisha kura.
 
Mabomu yameletwa mengine na wanaendelea kuyamwaga kama njugu. Kibaya zaidi, sasa polisi wanawakimbiza watu hadi mitaani mbali na ofisi ya Mkurugenzi na hata wakikuta wamesimama zaidi ya mmoja wanawarushia bomu.
Nasikia Blandes alikuwa ameishakubali kushindwa na kuamua kuondoka tangu jana, lakini wenye mamlaka wamemuita arudi ili wamsaidie.
 

Swali dogo tuu, hivy vyama vinahakikisha matokeo kwa kutumia nakala walizopewa wakala toka vituoni au wanategema tuu TUME itende haki kama wana huo utashi?
 
Hao wanaokimbizwa si ndio wapiga kura wenyewe? Hii inji imeisha sasa.
 
Habari ni kwamba watu wamepigwa vibaya na wengine wamekimbizwa hospitali.... Mtu waliyemchagua asiwe mbuge!!! Hiyo ndiyo demokrasia ya Demokrasia. Sitashangaa JK akitangazwa ushindi wa kishindo wa 100%+
 
Watabana lakini wataachia tu pengine wana-test Dhali
 
Habari ni kwamba watu wamepigwa vibaya na wengine wamekimbizwa hospitali.... Mtu waliyemchagua asiwe mbuge!!! Hiyo ndiyo demokrasia ya Demokrasia. Sitashangaa JK akitangazwa ushindi wa kishindo wa 100%+

Wewe F.a.la si Ulisema Kwamba Mgombea wa CHADEMA ametangazwa na Watu wanashangalia?
 
CCM ni zaidi ya magaidi. Wanastahili kuishi Yemen tu...hapa wapo kwa bahati mbaya
 
Afu hawa polisi ni wapuuzi kweli,hawana akili hata kidogo...badala wamuache mpiganaji apite ili aje awasaidie coz wana shida kibao!
Look at their houses...


Mbona mawakili wanawatetea mafisadi?
 
ccm kuanchia majimbo kwao ni issue

issue kubwa na saizi huyu msomali anatangaza majimbo 29 kwa wapinzani na mengine kwa ccm wakati bado mengine hayajatangazwa........ Somalia hiyo!
 
Jamani inabidi viongozi wa Chadema waingilie katika suala hili. Huwezi kuachia watu wanapigwa mabomu ili kumfanya mtu fulani ashinde. Nini kinaendelea huko. Kama akina Mnyika na wengine wanasikia tafadhali ili ni suala la kufuatilia na kulitolea tamko katika vyombo vya habari haraka sana.
 
Si kule kuna MKuu wa WIlaya MASAWE RAfiki wa kikwete toka University
 
Nimeongea na jamaa yangu kanambia ni kama yeboyebo hawataki yatangazwe wakisubiri amri na maelekezo toka "makao makuu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…